JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA?

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA?

➡️ Post

Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada ya kujifungua kabla haujapata mzunguko mwingine wa hedhi. Hii ni kwa sababu, yai la mwanamke huwa linapevuka wiki mbili kabla ya kupata hedhi, yaani siku ya kumi na nne kabla ya tarehe ya kwanza ya kupata hedhi, 


kwa maana hiyo yai linaweza kupevuka na kuweza kuwa kwenye hatari ya kupata ujauzito bila wewe kutambua. Kwa sababu, kupata kwa hedhi ni matokeo ya yai kutopevushwa.


Kimsingi, ni ngumu kwa mama mjamzito kupata mimba mara tu baada ya kujifungua, hasa kama unanyonyesha vizuri.


Hii ni kwa sababu, kuna vichocheo au homoni ambazo hutolewa kipindi cha kunyonyesha ambayo huzuia yai kupevuka kwa yai na kusababisha kukosa hedhi kwa miezi kadhaa, kitaalamu lactational Amenorrhea. 


Kukosa huku hedhi hakukukingi kwa asilimia mia moja kupata ujauzito ndio maana ukijifungua kwenye vituo vya afya au hospitali huwa unashauriwa kuhusu njia bora za uzazi wa mpango pale utakapokuwa tayari kuanza tena kufanya tendo la ndoa.


Wakina mama wengi huwa wanapenda kusubiri kupewa ruhusa na daktari wake wakati wanapoenda kliniki baada ya kujifungua, ingawa wapo ambao huwa wanajisikia wako tayari pale tu damu inapokata au nyuzi na michubukuko ya kupindi cha kujifungua vinapopona.


Kama unanyonyesha na kutumia maziwa ya kopo, hedhi inaweza kurudi baada ya wiki sita mpaka kumi baada ya mtoto kuzaliwa. 


Kama ni kunyonyesha peke yake inaweza kuchukua kipindi kirefu Zaidi yaani miezi kadhaa, ingawa hamna jibu la moja kwa moja kuhusu  ni lini au ni kipindi kipi unaweza kupata hedhi.


Ni vyema kupata ushauri wa daktarin hata kama ni siku za awali baada ya kujifungua, ili kuweza kupanga mapema na kuamua.


Je naweza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango wakati nanyonyesha?


Katika miezi sita ya mwanzo huwa haishauriwi kutumia vidonge vya uzazi wa mpango vyenye mchanganyiko wa homoni au vichocheo kwa maana huweza kupunguza kiasi cha maziwa ambacho hutolewa. Ingawa kutumia kidonge chenye kichocheo aina moja kitaalamu Progesterone only pill huwa ni salama kabisa. 

 @afyadarasa @afyabongo @afyaclass

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!