KANSA YA INI
.........
KANSA YA INI,DALILI ZAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE
Katika mwili wa Binadamu kuna aina nyingi za Kansa Ikiwemo hii ya ini ambayo tunaizungumzia hivi Leo. Kansa hizo ni pamoja na;
- Kansa ya Damu
- Kansa ya Ngozi
- Kansa ya Mapafu
- Kansa ya Koo
- Kansa ya utumbo
- Kansa ya shingo ya Kizazi
- Kansa ya matiti
- Kansa ya kizazi
- Kansa ya Ini
- Kansa ya Ubongo
- N.K
Hivi leo tutazungumzia kuhusu aina hii ya kansa ya ini,Je dalili zake ni zipi? na matibabu yake ni yapi?
Kama lilivyo neno lenyewe,Kansa hii hutokea kwenye ini, na endapo itatokea Mgonjwa atapata Dalili zifuatazo;
- Mgonjwa kuanza kutoa Damu puani
- Mgonjwa kujisaidia kinyesi chenye rangi nyeusi
- Mgonjwa kukojoa Mkojo wenye rangi nyeusi
- Mgonjwa kuanza kupata maumivu ya viungo mbali mbali ikiwemo na mabega
- Mgonjwa kushindwa kushiriki vizuri tendo la Ndoa
- Mgonjwa kuanza taratibu kupoteza kumbukumbu zake
- Mgonjwa kuingiwa na hali ya kukosa usingizi mara kwa mara
- Mapigo ya moyo ya mgonjwa kwenda mbio
- Kupatwa na hali ya kubadilika rangi kwenye macho pamoja na Ngozi ya mwili kuwa MANJANO kitaalam hujulikana kama JAUNDICE
- Kupatwa na maumivu makali ya Tumbo juu kidogo ya kitovu
- Mgonjwa kukosa hamu ya kula kabsa
- Mwili kuchoka kupita kiasi pamoja na kuhisi kichefuchefu
MATIBABU
Kama zilivyo kansa zingine,urahisi wa matibabu ni pale ambapo ugonjwa huu umegundulika mapema kabla ya kufikia stage mbaya,Kwani ikifikia stage mbaya hata kutibu pia ni vigumu. Hivo pale ukijihisi tofauti pamoja na kuona dalili nilizozitaja hapo juu wahi hospital kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
muhimu
new
post
uzazi
videos
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!