KANSA YA TUMBO,DALILI ZAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE

  KANSA YA TUMBO

.........

KANSA YA TUMBO,DALILI ZAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE


Katika mwili wa Binadamu kuna aina nyingi za Kansa Ikiwemo hii ya tumbo ambayo tunaizungumzia hivi Leo. Kansa hizo ni pamoja na;


  1. Kansa ya Damu
  2. Kansa ya Ngozi
  3. Kansa ya Mapafu
  4. Kansa ya Koo
  5. Kansa ya utumbo
  6. Kansa ya shingo ya Kizazi
  7. Kansa ya matiti
  8. Kansa ya kizazi
  9. Kansa ya Ini
  10. Kansa ya Ubongo
  11. Kansa ya Tumbo
  12. N.K

Hivi leo tutazungumzia kuhusu aina hii ya kansa ya tumbo,Je dalili zake ni zipi? na matibabu yake ni yapi?


Kama lilivyo neno lenyewe,Kansa hii hutokea kwenye tumbo, na endapo itatokea Mgonjwa atapata Dalili zifuatazo;

  1. Kupatwa na Maumivu makali ya tumbo
  2. Kujisaidia kinyesi kilichochanganyika pamoja na Damu
  3. Kujisikia kichefuchefu na kutapika pia
  4. Mwili kuchoka kuliko kawaida
  5. Kupatwa na homa za mara kwa mara
  6. Kushuka kwa kasi kwa Uzito wa mwili
  7. Kupoteza kabsa hamu ya kula
  8. Wagonjwa hawa wapo pia katika hatari ya kupatwa na Shida ya utapiamlo
  9. Kupatwa na shida ya mvurugiko wa tumbo mara kwa mara ikiwa ni pamoja na Kuharisha,tumbo kujaa gesi n.k

MATIBABU

Kama zilivyo kansa zingine,urahisi wa matibabu ni pale ambapo ugonjwa huu umegundulika mapema kabla ya kufikia stage mbaya,Kwani ikifikia stage mbaya hata kutibu pia ni vigumu. Hivo pale ukijihisi tofauti pamoja na kuona dalili nilizozitaja hapo juu wahi hospital kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584






0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!