KANUNI MUHIMU ZA KUKUKINGA NA UTI
1:KOJOA/JISAFISHE KILA BAADA YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA
Utasaidia kuondoa bakteria na vijidudu vingine vya magonjwa ambavyo vinaweza kuwa viliingia kwenye mrija wa mkojo wakati unashiriki tendo la ndoa
-
2:JISAFISHE KUTOKA MBELE KWENDA NYUMA (Frontal to back wiping) kila baada ya haja kubwa na ndogo.Itasaidia kuzuia uingiaji wa bakteria ndani ya mrija wa mkojo kupitia uke.Utakuwa unajikinga pia na magonjwa hasa UTI ambao umekuwa ugonjwa sugu siku za hivi karibuni
-
3:WAKATI WA HAJA NDOGO UNAPASWA KUWA UMETULIA (Relaxed),mara nyingi kujisaidia huku umesimama au umejikunja kwa namna yoyote ile hubana misuli ya kibofu cha mkojo hivyo kusababisha kiasi fulani cha mkojo kibaki ndani.Hii husababisha athari kwenye kibofu cha mkojo pamoja na magonjwa hasa UTI.Wakati wa haja ndogo,jitahidi uchuchumae au ukae (kama choo ni cha kukaa)
-
4:HAKIKISHA MKOJO WOTE UNAISHA
Pia hakikisha huutunzi mkojo kwa muda mrefu.Unapofanya hivi wadudu hasa bakteria huzaliana kwa wingi sana.Unajiweka kwenye hatari ya kuugua magonjwa mengi hasa UTI
-
5:Baada ya kufanya mambo haya,hakikisha unavaa NGUO ZA NDANI zilizotengenezwa kwa pamba 100% pia uvae nguo zilizokauka ambazo hazikubani sana.Husaidia hewa inayopatikana kwenye uke na kibofu cha mkojo iwe imekauka.Nguo mbichi,zinazobana pamoja na nguo za ndani zilizotengenezwa kwa nylon au material yoyote ambayo SIYO ya pamba hutunza hewa yenye unyevu.Hali hii huchochea uzalianaji wa wadudu hasa bakteria hivyo kukufanya uwe unaugua mara kwa mara magonjwa mbalimbali hasa UTI.cc.afyainfo
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!