KARAFUU NA GESI TUMBONI,HARUFU YA KINYWA,KIKOHOZI
KARAFUU
• • • • • •
Karafuu ni tiba nzuri ya kuondoa gesi tumboni,harufu mbaya ya kinywa,kikohozi pamoja na kuondoa/kupunguza kabisa maumivu ya meno. Hii inatokana na uwepo mwingi wa kemikali za eugenol ambazo kwa karafuu halisi,huchukua zaidi ya 90% ya kemikali zote.
-
Kwa kuondoa gesi tumboni,harufu mbaya ya kinywa pamoja na kikohozi hufaa zaidi ikitumika kama kiungo cha chakula,au hata kwa kutafuna.
-
Kwa matumizi ya kuondoa maumivu makali ya meno,mafuta yake ndiyo mazuri zaidi.Unapaswa kulowanisha pamba na mafua haya kisha iweke sehemu iliyo na tatizo (pia kama kuna shimo) kwa dakika 15,fanya hivyo mara 2 kwa siku kila mara na utaona matokeo yake.
Kitu cha muhimu kukumbuka ni kuitoa hiyo pamba baada ya muda husika na utapaswa kuloweka tena kipande kingine kidogo cha pamba wakati utapoamua kufanya zoezi hili.Kwa asiye na mafuta,anaweza pia kuitafuna tu!
Cc; afyainfo
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!