KUACHIA KWA KONDO LA NYUMA(PLACENTA ABRUPTION),SABABU,DALILI NA MADHARA YAKE KWA MJAMZITO
KUACHIA KWA KONDO LA NYUMA(PLACENTA ABRUPTION),SABABU,DALILI NA MADHARA YAKE KWA MJAMZITO
KONDO LA NYUMA KUACHIA
Hii ni moja ya dalili za hatari kwa mama Mjamzito na ambayo inataka msaada wa haraka sana.
Tatizo hili huhusisha placenta au kondo la nyuma kuachia sehemu lilipojishikiza na kusababisha madhara makubwa kwa mama mjamzito pamoja na mtoto aliyetumboni.
VISABABISHI VYA TATIZO HILI LA KUACHIA KWA KONDO LA NYUMA
✓ Kuwa na tatizo la Presha ya kudumu yaani kwa kitaalam huitwa Chronic Hypertension
✓ Kuwa na tatizo la Kifafa cha mimba
✓ Kuwa na tatizo la presha inayotokea wakati wa Ujauzito yaani kwa kitaalam huitwa Pregnancy Induced hypertension
✓ Chupa ya mama Mjamzito kupasuka mapema yaani Premature rupture of membrane
✓ Kupatwa na ajali ya kudondoka ama kupigwa wakati wa ujauzito
✓ Kuwa na historia ya tatizo hili la kondo la nyuma kuachia katika Ujauzito uliopita,upo kwenye hatari ya hali hii kujirudia tena
DALILI ZA TATIZO HILI LA KONDO LA NYUMA KUACHIA
- Mama mjamzito kuvuja damu hasa hasa ambayo ni nyeusi.
- Hali ya Mtoto aliye tumboni kuanza kubadilika gafla
- Tumbo kuanza kukaza na kuwa gumu
MATIBABU
Matibabu sahihi na salama ya tatizo hili ni mama kufanyiwa upasuaji wa haraka na mtoto kutolewa tumboni.
MADHARA YA TATIZO HILI
Ni pamoja na;
- Mama kupatwa na hemorrage shock
- Mtoto kufia tumboni
- Kuzaa mtoto kabla ya wakati wake
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!