KUPATA GANZI MIGUUNI

TATIZO LA KUPATA GANZI MIGUUNI

Mtu huweza kuhisi ganzi (numbness) miguuni kutokana na kukaa mkao ambao unaongeza mgandamizo kwenye mishipa ya fahamu (nerves) au kupunguza mtiririko wa damu (bloodflow).

.

Lakini pia kuhisi ganzi kwa muda mrefu zaidi isivyo kawaida kunaweza kuashiria uwepo wa magonjwa sugu mwilini kama; Kisukari, Kiharusi, Fibromyalgia, Peripheral Artery Disease n.k... .

.

KUMUONA DAKTARI

Unaweza kumuona daktari kama utakuwa na ganzi endelevu au zinazo ambatana na dalili zifuatazo;

1. Kuchanganyikiwa 

2. Kushindwa kupumua 

3. Kizunguzungu 

4. Kushindwa kubana mkojo

5. Ganzi inayohusisha viungo vingi mwilini ama mwili mzima

6. Ganzi iliyoanza baada ya jeraha la kichwa

7. Maumivu makali ya kichwa

8. Kushindwa kupumua .

.

NINI CHA KUFANYA?

Kama umekaa mkao fulani jaribu kubadilisha na kama una ganzi endelevu au yenye kuambatana na dalili tajwa hapo juu, Fika Hospitali. 

 #drtareeq #afyaclass


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!