KUPATA HEDHI KILA MWEZI HAKUTOI UHAKIKA WA WEWE KUPATA MIMBA

HEDHI

• • • • • •

Kupata hedhi kila mwezi hakutoi uhakika wa nafasi sawa ya kupata ujauzito. Wakati mwingine,hedhi ya mwanamke huwa ni matokeo ya damu na uchafu unaotokana na kubomoka kwa mji wa uzazi bila hata kuwepo kwa yai kwenye mwezi husika. Hii inamaanisha kuwa,mwanamke anaweza kupata hedhi lakini asiwe ametoa yai kwenye mwezi huo. Kitendo cha mwanamke kupata hedhi bila kutoa yai/mayai huitwa anovulation. Hutoa ishara ya kuwa mzunguko wa hedhi wa mwezi huo ulifanyika vizuri,lakini yai halikutolewa

-

Mojawapo ya sababu ya kutokea kwa hali hii ni mwanamke kushiriki kazi au mazoezi magumu sana (mfano kubeba vyuma),wasiwasi mkubwa na msongo wa mawazo,mvurugiko wa homoni hasa uwepo wa kiasi kikubwa cha homoni ya prolactin,uzito mdogo,kiribatumbo,matatizo kwenye vifuko vya uzazi pamoja na uwepo wa changamoto fulani kwenye tezi za thyroid

-

Hili linaweza kuwa jawabu kwa wanawake wanaohangaika kupata watoto huku hedhi zao zikitokea kila mwezi. Pengine hutoi mayai,fika hospitalini uchunguzwe na kusaidiwa!

#afyasolution




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!