Ticker

6/recent/ticker-posts

KUTOKEA KWA HOMA(FEVER)



HOMA(FEVER)


Imeandaliwa na doktamathew


Habarini za mchana mabibi na mabwana,Leo naomba nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu neno homa..homa inaeza kusababishwa kwa asilimia kubwa na magonjwa ya kuambukiza ,saratani,magonjwa ya mwili kujishambulia mwenyewe nk

Homa sio kitu kingine kama inavyotumika mtaani mfano mtu akiumwa kichwa anasema ana homa nk

Homa ni ile hali ya joto la mwili kua juu zaidi ya joto ambalo linatakiwa kikawaida.. Kikawaida joto la mwili linatakiwa kua kati ya nyuzijoto 35.5 hadi 37,ikizid 37 tunaanza kusema una homa.

Kuna aina 2 za homa  ambazo ni homa la kawaida na homa kalisana(joto zaidi ya nyuzijoto 38.5)


Zipo njia kadhaa za kupima joto.

1) kuweka kipima joto kwapani.

2) kuweka kipima joto chini ya ulimi

3) kuweka kipima joto kwenye mkundu

4) kuweka kipima joto kwenye sikio


Njia zote zinapima joto lakini zenye majibu ya uhakika zaidi ni njia Namba 3

Mtu mwenye homa atakua anajisikia kua na mwili Wa moto sana,anakua anatoa jasho,mwili kuchoka,moyo kwenda mbio,kupumua haraka haraka nk.

Joto likiwa Kali sana na lisiposhushwa basi  llaweza kuleta madhara makubwa kama kupata degedege,kuzimia na hata kufa.

Zipo njia nyingi za kushusha joto ambalo liko juu kama kuvua nguo zote(inafanyika kwa watoto sana sana),kuoga,kutumia dawa kama paracetamol, ibuprofen nk.

Joto linapokua lipo tu haliishi nakusihi muone mtaalamu Wa afya ili aweze kutibu kile kinachosababisha homa.. NAAMINI SASA NIMEELEWEKA NA UNAJUA NINI MAANA YA HOMA... KAMA BADO HUJAELEWA ULIZA SWALI HAPO CHINI

.

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





Post a Comment

0 Comments