KUTOKWA NA MAJIMAJI KWENYE MATITI(GALACTORRHEA)

MATITI

• • • • • •

Kutokwa Na Majimaji Kwenye Matiti (Galactorrhea)


Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba.Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale  yanapotoka wakati mwanamke hana historia ya dalili hizo hapo juu.


Tatizo hili huwapata wanawake wengi na kwa mujibu wa takwimu huathiri asilimia tano hadi 32 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa.Pamoja na kuwapata zaidi wanawake, hali ya kutokwa na majimaji katika matiti pia huweza kuwatokea wanaume watu wazima, vijana walio katika umri wa balehe, wa kike na wa kiume, watoto wachanga wa kike na wa kiume.


Chanzo cha tatizo

Matiti yanaweza kutoa majimaji endapo chuchu zitachezewa au kunyonywa mara kwa mara na kusababisha kuvuruga baadhi ya


 homoni mwilini.

Homoni zinazohusika zaidi na tatizo hili ni homoni ya ‘prolactine’.

Vilevile katika hali hii ya kutokwa na majimaji asilimia 50 ya matatizo chanzo chake bado hakijulikani.


Mama anayenyonyesha homoni zinazochangizwa na kusababisha matiti yatoe maziwa ni ‘Prolactin’, Estrogen’ na


 Progesterone.

Dawa nyingine zinazoweza kumfanya mtu atokwe na majimaji katika matiti ni dawa kama Methyldopa, madawa ya kulevya na dawa za magonjwa ya akili.


Pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni, hali ya kusuguasugua kifua mara kwa mara, hali ya kuwa na hofu na wasiwasi au shauku f’lani, mfano ya kuhitaji kupata ujauzito husababisha kuamsha homoni za uzalishaji wa maziwa au hayo majimaji.


Vyanzo vingine ni matatizo kichwani kwenye tezi ya ‘pituitary au pituitary adenoma’.

Dawa nyingine zinazoamsha tatizo hili ni kama vile ‘Cimetidine’ ambazo hutibu vidonda vya tumbo.


Kwa ujumla tatizo hili husababisha ugumba.

Kwa vijana na watoto wa kiume au wa kike ni vema uchunguzi wa kina ufanyike.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!