NYOKA
• • • • • •
KUUMWA NA NYOKA
DALILI
crotalinae husababisha
1. Kuvimba
2. Maumivu makali mfanano wa kuungua na moto
3. Kuvilia damu
4. Malengelenge
5. Iwapo matibabu yatachelewa hupelekea kuoza kwa eneo husika
Dalili nyingine ni
6. Kichefu chefu na kutapika
7. Shida katika kuona
8. Ladha ya chuma mdomoni
9. Kukakamaa kwa misuli
Elapidae husababisha
1. Kushindwa kupumua
2. Kushindwa kufanya kazi kwa milango ya fahamu
3. Kupooza kwa sehemu mbalimbali za mwili
NINI KIFANYIKE BAADA YA KUUMWA NA NYOKA.
Ziko njia mbalimbali za asili/ tiba mbadala ambazo zimekuwa zikitumika. Baadhi ya njia hizi zinapingwa kitaalamu na badhi zinafanyiwa uchunguzi. Njia kama kuchana chana kidonda, kuweka manyoya ya ndege au kutumia denge, kunyonya sumu, kufunga kamba na nyinginezo zimeonekana kuwa na madhara zaidi ya faida hivyo zinapingwa na wataalamu.
Iwapo mtu ameumwa na nyoka haraka fanya yafuatayo.
1. Toka/ mtoe eneo ambapo tukio imetokea
2. Ondoa kigu chochote kinachobana eneo hilo kuzuia madhara iwapo uvimbe utatokea. Tambua nyoka wengi wenye sumu hawasababishi vifo.
3. Epuka kutumia njia za asili
4. Safisha kidonda kisha nyanyua eneo husika juu ya usawa wa moyo na kisha haraka muwaishe hospitali. Huko matibabu yatafanyika kama inavyostahiri.
By Emmanuel Lwamayanga
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!