KUUMWA NA NYOKA,WATU WALIOKATIKA HATARI,NINI HUTOKEA UUMWAPO NA NYOKA

NYOKA

• • • • • •

KUUMWA NA NYOKA. 

janga hili linazikumba jamii nyingi zilizo kwenye maeneo ya joto kote duniani.  Takribani vifo 125,000 hutokea dunian kwa mwaka kufatia kuumwa na nyoka wenye sumu


WATU WALIOKATIKA HATARI

1. Wavuvi

2. Wawindaji

3. Wakulima vijijini

4. Watoto wadogo

5. Watu wanaoishi kwenye mazingira/nyumba duni na wasio na elimu ya kujikinga na wasio na huduma za afya katika maeneo yao. 

Nyoka wenye sumu huweza kugawanywa kwenye makundi makuu mawili nayo kitaalamu ni 

1. Crotalinae

2. Elapidae

Hii ni kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika hasa marekani. 

Tofauti za makundi haya ni, 

1. Crotalinae

Nyoka hawa sifa zao ni

- wana vichwa vya pembe tatu

- mboni za macho yao huwa mfano wa mviringo husio sawa

- wanavishimo joto usoni

- wana chonge/meno makubwa mfano wa msitatili kwa mbele. 

2. Elapidae

Nyoka hawa sifa zao ni

- wana vichwa vya duara

- mboni zao ni za mviringo

- hawana chonge

- wamegawanyika katika makundi makuu matatu. 

Ajari za kuumwa na nyoka hasa miguuni ni nyingi sana. 


NINI HUTOKEA UUMWAPO NA NYOKA. 


nyoka katika kundi la crotalinae huweka sumu zao chini ya ngozi ya binadamu wamuumapo yaani katika ukanda/tishu wa mafuta.  Mara chache sumu huweza fika kwenye misuli na hivyo kupelekea kufa kwa seli na kuoza kwa eneo ilo na hata shida katika mfumo wa mzunguko wa damu. Sumu hizi zinamadhara katika damu. 


Iwapo sumu itapelekea kuharibika na kuvuja kwa mishipa midogo ya damu, hali hii huweza kupelekea kukusanyika kwa majimaji ktk mapafu na mfumo mzima wa upumuaji, shinikizo la chini la damu nk. Pia sumu hizi zinaweza pelekea kuharibika kwa mfumo mzima wa ugandaji wa damu na hivyo kupelekea kutokwa na damu nyingi. 


Sumu hizi zina vijenzi vya protini amino asidi,  mafuta wanga na madini mbalimbali yakiwemo zinc. Protein hizi hupelekea kuharibika kwa ukuta ulindao seli,  viunganishi vya seli na hivyo kuleta madhara makubwa mwilini. Madhara yanategemea wingi/kiwango na ubora wa sumu yenyewe. 


Sumu za elapidae zinavijenzi ambavyo hushambulia mfumo mzima wa fahamu na hivyo kusababisha madhara makubwa ndani ya muda mfupi ikiwemo kushindwa kupumua. 

By Emmanuel Lwamayanga




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!