MBU+UKIMWI
• • • • • •
KWANINI MBU HAWEZI SAMBAZA UKIMWI.
wakati wa nyuma wakati gonjwa hili limeibuka watu wengi walikuwa na uoga sana huku wakiamini kwakuwa mbu anaishi kwa damu basi atakuwa na uwezo wa kusambaza UKIMWI iwapo atafyonza damu ya muathirika na baadae kufyoza damu ya asiyemuathirika.
Tafiti mbalimbali zilifanyika katika hili na ikagundulika kuwa mbu hana uwezo wa kusambaza/kuambukiza UKIMWI.
MIONGONI MWA SABABU NI?
1.sifa inayomfanya kirusi wa UKIMWI kuwa hatari kwa binadamu ni uwezo wake wa kuingia, kujificha na hata kuzaliana katika aina ya seli/chembe chembe nyeupe za damu kitaalamu zinafahamika kama T4 lymphocytes. Na ili kirusi huyu haweze kuingia katika seli hizi lazima kuwe na vitu vya kumpokea kitaalamu huitwa receptors. Seli nyingi zinazoshambuliwa na kirusi cha UKIMWI kina kipokeo kiitwacho CD 4. MBU na wadudu wengine wengi hawana aina hii ya seli hivyo virusi vya UKIMWI haviwezi kuishi katika mwili wa mbu na kwa mantiki hiyo uharibiwa na kemikali zilizo katika tumbo la mbu.
2. Wengi tunaamini kuwa mdomo anaotumia mbu kufyonza damu na kutema mate yenye vimelea ni ule ule, HAPANA. mdomo wa mbu umegawanyika katika sshemu mbili moja huusika katika kufyonza damu na nyingine kutema mate na mate hayo huwa yanakemikali ambayo kwa maneno ya kawaida hutumika kuyeyusha damu na hivyo kumsaidia kufyonza damu kwa urahisi. Vimelea vya malaria viko na uwezo wa kupenya kutoka tumboni mwa mbu na kuingia kwenye tezi za mate na hivyo kuweza kusambazwa na mbu lakini kirusi cha UKIMWI hakina uwezo wa kujipenyeza katika kuta hizo kwasababu hakuna vipokeo yaani receptors ambazo hutambuliwa na kirusi huyo katika mbu.
3. Katika hali ya kawaida kwa muathirika, damu yake huwa na kiwango kidogo cha virusi. Hivyo basi hata kama mbu atafyonza damu hiyo basi damu hiyo itakuwa na kiwango kidogo sana cha virusi ambao hawatakuwa na uwezo wa kusababisha maambukizi
4. Kiwango kidogo cha virusi katika damu pia ni sababu inayoeleza kwann mbu hawezi sambaza gonjwa hili kwa mabaki ya damu yanayobaki mdomoni kwake. Kitaalamu ili mbu aweze kufikisha kiwango cha virusi vitakavyoweza kusababisha UKIMWI basi mbu milioni 10 waliofyoza damu ya waathirika wamuume mtu kwa wakati mmoja.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!