LIJUE KONDO LA NYUMA AU PLACENTA

KONDO LA NYUMA

• • • • • •

Hili kwenye picha ndio linaitwa kondo la nyuma kitaalamu inaitwa “placenta”


Linapatikana kwa Mama,katika Mfuko wa Uzazi na pia linajihusisha na kazi nyingi za Uzazi.


Kondo la nyuma linakazi nyingi ikiwemo

1. Kusafirisha virutubisho na taka mwili baina ya mama na mtoto alietumboni. Miongoni mwa vitu ambavyo usafirishwa ni oksijen, carbon dioxide, taka mwili kama  urea, uric acid na creatinine. Mtoto hupokea sukari, mafuta, amini asidi, maji na madini, vitamini na homoni kutoka kwa mama kupitia kondo la nyuma.


2. Pia humkinga mtoto kutokana na vitu hatarishi awapo tumboni


3. Kondo la nyuma hutengeneza homoni mbalimbali ambazo husaidia kulinda na kuboresha mimba.


Je wajua kwamba mpaka kipimo cha Mimba Kwa Njia ya Mkojo yaani Urinary Pregnancy test (UPT) kisome ni lazima kondo la Nyuma(placenta) lizalishe kichecheo kinachoitwa human gonadotrophin Hormone(hcg) kwenye Mkojo?


Hizo zote ni kazi za Kondo la Nyuma au Placenta


Mimba itakuwa kwenye hatari endapo kondo la nyuma limeachia yaani Placenta abruption au Kujishikiza sehemu ya chini na kufunika mlango wa uzazi yaani Placenta praevia.


Ambapo mwanamke atapata dalili mbali mbali kama maumivu ya tumbo,damu kutoka wakati wa Ujauzito n.k





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!