MADHARA AU MATOKEO MABAYA YA MAKOVU KWENYE NJIA YA MKOJO
NJIA YA MKOJO
• • • • • •
MADHARA AU MATOKEO MABAYA YA MAKOVU KWENYE NJIA YA MKOJO
Kama makovu yakiachwa bila kutibiwa yanaweza kulete madhara au matokeo yafuatayo
1)Kupata mawe kwenye kibofu cha mkojo(bladder stones)
2)Kupata UTI za mara kwa mara (urinary tract infections)
3)Mafigo kuvimba/kujaa(hydronephrosis)
4 Kutoa mkojo kwenye mapaja,chini ya uume(urethral fistula)
5)Majipu kwenye njia ya mkojo na maeneo jirani(periurethral abscess)
NAMNA MAKOVU KWENYE NJIA YA MKOJO HUGUNDULIKA
Makovu kwenye njia ya mkojo huhisiwa na hubainika kwa kusikia historia aitoayo mgonjwa kwa kuzingatia dalili tajwa hapo juu. Mara baada ya kusikia dalili hizo basi mtaalam wa afya anaweza kukuandikia baadhi ya vipimo ili kubaini tatizo lako na kama kuna madhara yeyote yametokea. Daktari kulingana na hali na maelezo ya mgonjwa anaweza kuandika vipimo kama x ray maalumu ya kuangalia njia ya mkojo(retrograde urethrogram (RUG) na voiding cystourethrogram (VCUG)),kipimo kama ultrasound , cystourethroscopy na uroflowmetry
MATIBABU YA MAKOVU KWENYE NJIA YA MKOJO
Matibabu ya mkovu kwenye njia ya mkojo yapo na hutegemea na hali ya mgonjwa,ukubwa na urefu wa kovu lenyewe na kama kuna madhara yeyote yametokea. Kama mgonjwa akija akiwa na hali ya dharura basi italazimu atobolewe kwenye tumbo kwa chini ili awekewe mpira wa mkojo(urinary diversion procedures) ,kutobolewa chini ya makende ilie mkojo utoke (perineal urethrostomy) Pamoja na kupewa daw za kuua vimelea.
Ikumbukwe kwamba makovu madogo ambayo hayana dalili yeyote kwa mgonjwa basi hayahitaji matibabu kwa haraka bali huhitaji kufuatliwa kwa ukaribu ili kuona kama kovu linaongezeka au la. Kwa makovu makubwa na yenye dalili hufanyiwa baadhi ya tiba kama kutanua njia ya mkojo(dilatation),kukata n kuondoa sehemu ya njia ya mkojo yenye kovu(urethrotomy na kuondoa kovu na kupandikiza tishu mpya ambayo itakua njia mpya ya mkojo isokua na kovu(urethroplasty.
#doktamathew
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!