MADHARA YA KUPAKA LIPSTICK MDOMONI

 YAJUE MADHARA YA KUPAKA LIPSTICK MDOMONI

➡️ Lipstick

Lipstick ni aina ya urembo ambao huhusisha kupaka rangi za aina tofauti tofauti katika Lips za mdomo. Aina hii ya Urembo hutumiwa sana na Wanawake wengi Duniani kwa lengo la Kuongeza mvuto,urembo wa lips, n.k.

Historia ya Kupaka Lipstick ilianzia huko Nchini Misri ambapo, Mwanamke wa kimisri alikuwa anapaka Lipstick ya Rangi nyekundu kutambulisha na kuonyesha kwamba yupo tayari kwa ajili ya Kufanya Tendo la Ndoa,hivo ilikuwa Njia ya kupitisha Ujumbe kwa Mwanaume ili aweze kuelewa kwamba Mwanamke anahamu na Tendo hilo.

JE MADHARA YA KUPAKA LIPSTICK MDOMONI NI YAPI?

Tafiti zinaonyesha Madhara ya Lipstick hutokea sana sana pale Mwanamke anapomeza au kula chembechembe zinazotoka kwenye Lipstick, Na Madhara hayo ni Pamoja na;

- Kupatwa na matatizo ya Kansa au Saratani
- Tatizo la Midomo au lips kupasuka (Cheilitis)
- Kupatwa na Magonjwa ya Ngozi
- Mwanamke kupoteza mood
- Uchovu usiokuwa wa kawaida kwenye mwili pamoja na Maumivu makali ya Kichwa
- Magonjwa ya Figo
- Kupatwa na Shinikizo la Damu
- Kupatwa na hali ya kichefuchefu na kutapika mara kwa mara
- Kupatwa na Magonjwa ya mfumo wa Fahamu au Neva.


KUMBUKA; Hakuna mda maaulumu wa mtumiaji kuanza kupata Madhara haya, Bali kinga ni bora kuliko Tiba
.
.

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!