Connect with us

Uzazi/Ujauzito

MADHARA YA KUTOA MIMBA,Fahamu hapa Kila Kitu

Doctor Ombeni

Published

on

🩺
Medically reviewed by Afyaclass Teams,Gynecologists
242 Views
0 Comments

YAFAHAMU MADHARA AMBAYO MTU HUWEZA KUPATA BAADA YA KUTOA MIMBA

Madhara gani mtu anaweza kupata kwakutoa mimba au ujauzito?

Kitendo hiki ni hatari sana kwa afya yako.Madhara yatokanayo na utoaji mimba yapo mengi ila mimi ntataja baadhi tu kwa kukufungua macho ili ujue hatari ya kitendo hiki;

1.Mji wa uzazi kushindwa kukakamaa(contracts) mara baada ya kutoa mimba hivyo kusababisha damu nyingi kutoka na kupelekea kupoteza MAISHA kwa mhusika.

2.Maambukizi yanayotokana na vimelea mbalimbali vya magonjwa kama vile bacteria vinavyoingia katika mji wa uzazi wakati wa kutoa mimba ambavyo huweza kusambaa mwili mzima kuleta maambukizi ya vimelea hivyo kwenye damu(Sepsis).

3.Kuumia au kutoboka kwa viungo vya mwili Kama vile;

  • mji wa mimba,
  • kibofu cha mkojo,
  • utumbo,na hata figo

kunakosababishwa na matumizi ya vitu venye ncha kali katika kutoa mimba Kama vile vijiti, n.k..

4.Kubaki kwa masalia ya mimba ndani ya mji wa uzazi, ambayo huongeza hatari ya mama kuvuja damu nyingi na hata kupoteza Maisha.

5.Kupoteza kabisa uwezo wa kuzaa au kushika mimba hivo kuwa kilio cha Maisha. Hasa ikiwa njia zilizotumika sio sahihi au zimesababisha madhara zaidi..

Je,Unachangamoto yoyote ya Kiafya?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Madhara mengine ya kutoa mimba 

Wanawake wengi huanza kukutana na matatizo haya baada ya kutoa Mimba;

– Kuvuja damu sana na kwa muda mrefu

– Kupata maumivu ya tumbo mara kwa mara, tumbo kukaza n.k

– Kupata shida ya kizunguzungu au hata kuzimia

– Kupata kichefuchefu na kutapika n.k

Dalili hizi huweza kuisha zenyewe ndani ya wiki ila wakati mwngine huweza kuwa tatizo la Muda mrefu.

Article Review-Madhara ya kutoa mimba changa

Haya hapa ni Madhara ambayo huweza kutokea kwa Mtu kutoa Mimba;

1. Kuharibika kwa Kizazi au shingo ya kizazi(womb/cervix)

2. Kupata tatizo la kuvuja damu kupita kiasi

3. Mimba kutoka na kuacha mabaki mengine ndani(Incomplete abortion),

Hali hii ni ya hatari na inaweza kuleta madhara zaidi, hivo hatua za haraka ni muhimu,

Hii huweza kusababisha hata hatua kama (surgical abortion procedure) kufanyika.

4. Kupata maambukizi ya kizazi au mirija ya kizazi(uterus/fallopian tubes)

5. Kusababisha kovu au makovu ndani ya Kizazi

6. Kukuweka kwenye hatari Zaidi ya kupata maambukizi ya bacteria ambayo huingia moja kwa moja kwenye damu, na kisha kuleta madhara makubwa zaidi(Sepsis/Septic shock)

7. Kusababisha tatizo la kutoboka kwenye kizazi(Uterine perforation)

8. Utoaji Mimba Pia unaweza Kusababisha KIFO. n.k

Kwa Mujibu wa NCBI;

Zaidi ya asilimia 2% ya Wanaotoa Mimba hupata Matatizo kama vile;

  • Kupata Maumivu makali ya Tumbo
  • Kuvuja damu sana
  • Maambukizi ya magonjwa n.k

Utafiti wa NCBI unaendelea Kuonyesha; Na wengine hupata Madhara makubwa ikiwemo;

– Tatizo la misuli ya kizazi kushindwa kurudi mahali pake,tatizo ambalo kitaalam hujulikana kama uterine atony

– Kuvuja damu mvululizo(Subsequent hemorrhage)

– Kutoboka kwa Kizazi(uterine perforation),

– Kuumia kwa viungo vya karibu na kizazi kama vile; kibofu cha Mkojo au eneo la haja kubwa(injuries to adjacent organs (bladder or bowels),

– Kuchanika kwa mlango wa kizazi(cervical laceration),

– Mimba kushindwa kutoka, na kuleta madhara Zaidi(failed abortion),

– Kupata maambukizi hatari ya bacteria kwenye damu baada ya kutoa mimba( septic abortion)

– Kupata matatizo ya damu kuganda:disseminated intravascular coagulation.n.k

Kadri Mimba inavyokuwa kubwa Zaidi ndivyo hatari na madhara huongezeka Zaidi.

Maambukizi kwenye eneo la Via vya Uzazi(Pelvic Infection):

Bakteria (vijidudu) kutoka kwenye uke au mlango wa uzazi wanaweza kuingia kwenye uterasi na kusababisha maambukizi.

Matumizi ya Antibiotics yanaweza kusaidia kuondokana na maambukizi hayo.

Mimba kushindwa kutoka kabsa(Incomplete abortion):

Mabaki ya ujauzito kubaki ndani ya kizazi hali ambayo ni hatari Zaidi na huhitaji matibabu ya haraka.

Pia Utoaji mimba usio kamili unaweza kusababisha maambukizi na kutokwa na damu Zaidi.

Damu kuganda na kutengeneza Blood clots ndani ya kizazi:

Shida hii huweza kusababisha maumivu makali ya tumbo, lakini hatari zaidi ya kupoteza maisha, baada ya blood clots kusafiri kwenye damu mpaka kwenye mapafu na Kuziba.

Kuvuja damu kupita Kiasi:

Kutokwa na damu nyingi sio kawaida na kunaweza kusababisha madhara Zaidi.

Kuchanika kwa Mlango wa kizazi(cervix):

Kutoboka kwa kuta za kizazi(Perforation of the uterus wall:

Kifaa cha matibabu kinaweza kupitia ukuta wa uterasi na kutoa.Kwa Mujibu wa NCBI;

Kiwango kilichoripotiwa ni moja(1) kati ya kila utoaji mimba 500. Kulingana na ukali, utoboaji unaweza kusababisha maambukizi, kutokwa na damu nyingi au vyote viwili. Upasuaji unaweza kuhitajika ili kurekebisha tishu za uterasi, na katika hali mbaya zaidi kutoa kizazi chochote au hysterectomy inaweza kuhitajika.

Madhara Mengine ya Muda mrefu ya Kutoa Mimba ni pamoja na;

  • Mwanamke Kushindwa kubeba Mimba tena
  • kuwa kwenye hatari ya kupata Saratani za matiti,Ovari au kizazi(breast, ovarian and endometrial cancer).

Kupata madhara kisaikolojia(Emotional Side of an Abortion)

Unapaswa kujua kwamba wanawake hupata hisia tofauti baada ya kutoa mimba, Baadhi ya wanawake wanaweza kujisikia hatia, huzuni au kuwa na Msongo wa mawazo ambao hauishi baada ya kutoa Ujauzito,

wakati wengine wanaweza kuhisi utulivu kwamba utaratibu umekwisha. Baadhi ya wanawake wameripoti madhara makubwa ya kisaikolojia baada ya kutoa mimba, ikiwa ni pamoja na;

  • mfadhaiko,
  • huzuni,
  • wasiwasi,
  • kujidharau
  • majuto,
  • Woga
  • kurudi nyuma kwa kila kitu anchofanya
  • na kuingia kwenye matumizi mabaya ya dawa za kulevya.

Hisia hizi zinaweza kuonekana mara baada ya utoaji mimba au hatua kwa hatua kwa muda mrefu. Hisia hizi zinaweza kujirudia au kuhisiwa kuwa na nguvu zaidi wakati wa utoaji mimba mwingine, au kuzaa kwa kawaida, au siku ya kumbukumbu ya utoaji mimba.

Ikiwa haupati msaada na utegemezo wa familia, huenda ikawa vigumu kwako kukabiliana na hisia zinazotokea baada ya kutoa mimba.

Kuzungumza na mshauri wa kitaalamu kabla ya kutoa mimba kunaweza kumsaidia mwanamke kuelewa vyema uamuzi wake na hisia anazoweza kupata baada ya utaratibu huu, ili asikimbilie kufanya kitu ambacho hajui madhara yake.

Article Review&Summary:

Madhara ya kutoa mimba (abortion) hutegemea aina ya utoaji mimba, umri wa ujauzito, na hali ya afya ya mwanamke.

Madhara ya muda mfupi

  1. Kutokwa na damu ukeni.
  2. Maumivu au mikazo ya tumbo.
  3. Kichefuchefu, kutapika au kuhisi kizunguzungu.
  4. Maambukizi ya kizazi au mfumo wa uzazi ikiwa usafi haukuzingatiwa.
  5. Utoaji wa mimba kutokukamilika, hivyo kuhitaji matibabu zaidi.

Madhara makubwa yanayoweza kutokea

  1. Kutokwa na damu nyingi (hemorrhage).
  2. Jeraha au kuchanika kwa mfuko wa uzazi au shingo ya kizazi (hasa kwa njia za upasuaji zisizo salama).
  3. Maambukizi makali (sepsis), ambayo yanaweza kuhatarisha maisha.
  4. Kifo, hasa katika utoaji mimba usio salama.

Madhara ya muda mrefu

  1. Endapo kutatokea maambukizi makubwa yasiyotibiwa, yanaweza kusababisha matatizo ya uzazi.
  2. Msongo wa mawazo, huzuni au hisia za hatia kwa baadhi ya wanawake, ingawa si kila mtu hupitia hali hiyo.

References (APA)

  1. World Health Organization. (2022). Abortion care guideline. Geneva: WHO. https://www.who.int/publications/i/item/9789240039483
  2. World Health Organization. (2024). Abortion. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/abortion
  3. American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG). (2025). Induced Abortion. https://www.acog.org/womens-health/faqs/induced-abortion
  4. Centers for Disease Control and Prevention (CDC). Abortion Surveillance Reports. https://www.cdc.gov/reproductivehealth/data_stats/abortion.html
  5. Kwa Mujibu wa NCBI;
242 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

magonjwa1 year ago

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams,Gynecologists Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba Genital warts ni ugonjwa gani,Soma Zaidi hapa kufahamu Genital...

magonjwa2 years ago

Vipele Sehemu Ya Siri,Vipele Ukeni, Vipele Kwenye Uume

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams,Gynecologists VIPELE SEHEMU YA SIRI,VIPELE UKENI, VIPELE KWENYE UUME Vipele kwenye Uume: Vipele Kwenye Uume: Chanzo,...

magonjwa ya wanawake5 years ago

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams,Gynecologists  PID • • • • • PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya...

afyatips1 day ago

Dalili za kidonda cha operation kupona

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams,Gynecologists DALILI ZA KIDONDA CHA OPERATION KUPONA Baada ya kufanyiwa operation, mwili huanza mchakato wa kuponya...

Utafiti1 day ago

Desogestrel yahusishwa na Kuongezeka kwa Hatari ya uvimbe wa ubongo

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams,Gynecologists Mamlaka ya Dawa na Bidhaa za Afya ya Ufaransa (ANSM) imewaonya wanawake wanaotumia baadhi ya...

magonjwa5 years ago

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams,Gynecologists UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba) Huu ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama brucellosis na...

magonjwa ya watoto2 years ago

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams,Gynecologists Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga Ugonjwa wa Surua ni ugonjwa...

Afya News2 days ago

Vifo vya Watoto Wachanga Katika Mlipuko wa Surua Pennsylvania na Mjadala wa Afya ya Umma

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams,Gynecologists Mlipuko wa ugonjwa wa surua (measles) unaoendelea katika jimbo la Pennsylvania, Marekani, umeendelea kuzua wasiwasi...

Afya News2 days ago

Wauguzi Kenya Wasitisha Mgomo Baada ya Makubaliano na Serikali

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams,Gynecologists Wauguzi nchini Kenya wamesitisha mgomo wao wa siku 43 baada ya kufikia makubaliano na serikali...

WHO3 days ago

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams,Gynecologists Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa matumizi ya...

243
0