➖ HAYA NDYO MADHARA YA KUVUTA SIGARA
Kuna Kemikali zaidi ya 4,000 ndani ya Sigara ambazo zinaweza kudhuru mwili wa Mvutaji, Na kila sekunde 8, mtu mmoja hufariki dunia kutokana na matumizi ya Tumbaku (source: Wikipedia)
Madhara ya Matumizi ya Sigara ni Pamoja na haya yafuatayo;
1. Tatizo la nywele kunyonyoka- Hii ni kutokana na kwamba,uvutaji wa Sigara hudhoofisha kinga ya mwili na kupelekea mizizi ya nywele za Mvutaji kudhurika.
2. Kupata Magonjwa ya Macho- Tafiti zinaonyesha kwamba sehemu ya macho inayopunguza mwanga inaweza kufunikwa na kitu kama vile Wingu,hivo kusababisha hali ya upofu wa macho.
3. Matatizo ya Ngozi- Athari katika Ngozi hutokana na kemikali zilizopo kwenye Sigara, Hapa huhusisha ngozi kukuchanjamana, kwani kemikali hizo hupunguza uwezo wa ngozi kujirekebisha na kusababisha ngozi kuzeeka haraka na kupoteza uwezo wa kulainika.
4. Magonjwa ya Masikio- Sigara huweza kusababisha uwepo wa uchafu ambao huganda kwenye Mishipa ya Damu,hivo kupunguza uwezo wa damu kutembea ndani ya Sikio,na kuleta matatizo katika maskio ya mvutaji ikiwemo tatizo la kutokuskia Vizuri.
5. Saratani ya Ngozi- Kemikali zilizopo ndani ya Sigara huweza kusababisha Vidonda kwenye ngozi kutokupona haraka, na kueguka kuwa Saratani katika Ngozi.
6. Magonjwa ya meno- Sigara huweza kuongeza uchafu ambao unaganda kwenye Meno hivo kupelekea meno kuoza pamoja na harufu mbaya mdomoni.
7. Magonjwa ya Mapafu- Sigara huweza kusababisha Saratani ya mapafu,pamoja na Koromeo(koo), na pia kupasuka kwa vifuko vya hewa Ndani ya mapafu.
8. Matatizo ya Mifupa- kemikali ndani ya Sigara huweza kudhoofisha mifupa na kupunguza Nguvu katika mifupa.
9. Magonjwa ya Moyo- Uvutaji wa sigara huweza kusababisha,tatizo la shinikizo la Damu(Presha), mshtuko wa moyo,na kusababisha kifo pia.
10. Tatizo la Vidonda vya tumbo- Hii ni kutokana na kwamba,kemikali ndani ya sigara hupunguza uwezo wa tumbo kustahimili Acid baada ya kula,hivo kupelekea tatizo la Vidonda vya tumbo.
11. Madhara katika vidole,ikiwemo tatizo la kutu katika kucha na Vidole vya Mvutaji.
12. Ugonjwa wa Buerger- Huu ni uvimbe wa Mishipa ya Damu miguuni na mikononi ambapo tatizo hili lisipotibiwa haraka hupelekea kukatwa Mguu au mkono.
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!