UGUMBA
• • • • • •
MAGONJWA YANAYOWASABABISHA WANAWAKE KUWA WAGUMBA
1. P.I.D ni kifupishi Cha pelvic inflammatory Diseases
2. Fibroids au UVIMBE
3. U.T.I na FANGAS SUGU
P.I.D
- ni maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke na huweza kusababisha kuharibika kwa mayai,mirija ya uzazi au mfuko wa uzazi
✓ ugonjwa huu husababishwa na kutotibu MAGONJWA ya zinaa
DALILI KUU ZA P.I.D
• maumivu makali ya Tumbo chini au sehemu ya juu kulia
• kutokwa uchafu ukeni wenye harufu mbaya ambao wengi hudhani ni fangasi ila sio
• maumivu makali na kutokwa damu wakati wa tendo la ndoa
• UGUMBA unatafuta mtoto kwa muda mrefu bila mafanikio
• kutokwa na damu nyingi Sana wakati wa hedhi au hata wakati ambao sio wa hedhi
FIBROIDS / UVIMBE
- ni uvimbe ambao hutokea katika tumbo la uzazi ambako huweza kuwa ukutani mwa kizazi , Ndani kabisa ya kizazi au nje ya kizazi
DALILI KUU ZA FIBROIDS
✓ kutokwa damu nyingi katikati ya mwezi au kipindi Cha hedhi
✓ maumivu makali Sana ya kiuno kipindi Cha hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma huo uvimbe nje
✓ maumivu makali wakati wa tendo la ndoa mpaka kupelekea kuchukia kabisa
✓ Mimba kutoka mara kwa mara
✓ UGUMBA
✓ Kukojoa mara kwa mara
HONGERA KWA KUJIFUNZA MENGI
~ Kama umekumbwa na tatizo la UGUMBA tafuta suluhisho Sasa na ondoa zana ya ushirikina
~ kwa wanaume ukiona mke wako haoni raha kufanya mapenz na wewe msaidie yawezekana mwenzako anaumwa na moja Kati ya MAGONJWA haya na hajajua bado
~ Chukua hatua Sasa
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!