MAKOVU KWENYE NJIA YA MKOJO KWA WANAUME (URETHRAE STRICTURES)

MAKOVU KWENYE NJIA YA MKOJO KWA WANAUME  (URETHRAE STRICTURES)


Makovu kwenye njia ya mkojo yamekua yanaongezeka sana. Matatizo haya watu walio wengi wamekua hawayajui au hawayatilii maanani na mara nyingi mtu hugundulika ana tatizo pale anapokua anapata mawe kwenye njia ya mkojo pasipo kua na sababu nyingine yeyote.


VISABABISHI VYA MAKOVU KATIKA NJIA YA MKOJO


1)Kuumizwa wakati wa kuwekewa mpira wa mkojo (traumatic placement of indwelling urinary catheters)


2)Magonjwa wa zinaa (sexually transmitted disease)


3)Watu wanaopata tiba ya mionzi (radiation therapy)


4)Ugonjwa wa likeni (lichen sclerosus)


5)Wenye tatizo la kua na kitundu cha mkojo chini ya uume (hypospadias)


6)Ajali zinazogusa nyonga-hii ni kw nchi zinazoendelea (trauma in developing countries


7)Haijulikani hasa hasa kwa nchi zilzizoendelea (idiopathic in developed countries)---hii ni kwa asilimia 90 sababu inakua haijulikani


 


DALILI ZA AZIPATAZO MTU MWENYE MAKOVU KWENYE NJIA YA MKOJO


1) Kuumwa UTI mara kwa mara (recurrent urinary tract infections)


2)Kupungua nguvu ya kukojoa(decreased urinary stream)-hapa mwanaume anapokua anakojoa anakua hawezi kurusha mkojo mbali badala ya unaruka tu kwa karibu na akijaribu kusukuma kwa nguvu basi mkojo huruka mbali kwa nguvu.


3)Kupata maumivu wakati wa kukojoa(dysuria)


4)Kukoja mkojo uliojigawa kwa maana ya kua kama una mikojo Zaidi ya mmoja (urinary spraying)


5)Kushindwa kukojoa kabisa(BOO)-hii ni hali ya dharura sana ambayo huhitaji kutobolewa kwenye tumbo juu ya maeeneo ya mavuzi na kuwekewa mpira wa mkojo ili kutoa mkojo mabo umekataa kutoka(emergency transurethral or suprapubic catheter placement to facilitate urinary drainage)


6)Kupungua nguvu ya urukaji wa shahawa pale mwanaume afikiapo mshindo (decreased force of the ejaculate during orgasm)


7)Kuhisi kwamba mkojo haujatoka wote baada ya kukojoa(incomplete bladder emptying

Via Dr.mathew




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!