MATATIZO YANAYOMFANYA MWANAMKE ASIBEBE MIMBA KWA HARAKA

MIMBA

• • • • • •

MATATIZO  YANAYOMFANYA MWANAMKE  ASIBEBE  MIMBA KWA  HARAKA


Kwa kawaida mwanamke anatakiwa apate ujauzito ndani ya mwaka mmoja baada tu ya kuolewa au kuanza mahusiano na yule ambaye tayari ana mtoto.


Kitendo cha kukaa muda mrefu bila ya kupata mtoto huwa linahitaji kufanyiwa kazi.


CHANZO CHA TATIZO


Mwanamke kutopata ujauzito husababishwa na matatizo mengi kwa upande wake au mumewe.


Kwa upande wa mwanaume, vyanzo vinaweza kuwa kukosa nguvu kabisa au kupungukiwa nguvu za kiume tatizo liitwalo, ‘Erectile Dysfunction,’ 


Mwanaume anaweza kutoa manii mepesi sana kiasi kwamba baada tu ya kumaliza tendo mwanamke akisimama zinamwagika au zinatoka.


Dalili nyingine ni pale manii kuwa zipo chache sana au hazina nguvu ya kuogelea.


Kwa upande wa mwanamke, vyanzo vinaweza kuwa matatizo katika mfumo wa homoni au vichocheo mbalimbali vya uzalishaji na upevushaji mayai na mzunguko..


Mwanamke mwenye tatizo hili hupoteza siku zake za hedhi, mzunguko wa hedhi huvurugika na asijue ratiba yake ya mzunguko.


Pia hupoteza hamu na raha ya tendo, maumivu wakati wa tendo, hapati ute wa uzazi. 


Matatizo mengine ni kuziba kwa mirija ya uzazi, uwepo wa uvimbe katika mfuko wa uzazi (fibroids), kupata damu ya hedhi kwa muda mfupi sana yaani siku moja au mbili tu. Au pia kupata kwa siku nyingi mno (zaidi ya siku saba)


Pia kuumwa tumbo chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa sana na uchafu ukeni ambao wakati mwingine huambatana na harufu mbaya na muwasho pamoja na maumivu wakati wa haja ndogo.


Matatizo ya kutokwa na uchafu ukeni na muwasho havihusiani na ugonjwa wa yutiai ‘UTI’ kama wengi walivyozoea.


Matatizo mengine yanayomfanya mwanamke asipate ujauzito anapohitaji ni kutokufahamu siku za kupata mimba. Ili kufahamu siku za kupata mimba lazima ufahamu kwanza mzunguko wako uko vipi.


Vile vile mwanamke ajue siku zake za ‘Ovulation’ au siku za ute wa uzazi. 


::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!