MATATIZO YATOKANAYO NA UNYWAJI WA POMBE KIPINDI CHA UJAUZITO
Baadhi ya madhara yanayoweza kumpata kiumbe aliye tumboni kwa mama kutokana na unywaji wa pombe kipindi cha ujauzito ni pamoja na
Kutoka/kuharibika kwa mimba
Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo
Mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu wa mbavu na kidari (sternum)
Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya mgongo uliopinda (kibiongo) na vidole vilivyoundana
Mtoto kuzaliwa akiwa na kichwa kidogo kuliko kawaida (microcephaly)
Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya pua
Kuzaliwa na matatizo ya taya
Mtoto kuwa na matatizo ya kutokuona mbali
Matatizo ya moyo kama vile moyo kuwa na tundu
Matatizo ya figo
Mtoto kuwa na ubongo mdogo na pia matatizo ya akili
Mtoto kuzaliwa akiwa na mdomo sungura (lip palate na cleft palate)
Matatizo ya kimaumbile ya masikio na ulemavu kwenye sehemu za uzazi (genital malformations).
Aina mojawapo ya kansa ya chembe nyeupe za damu (Acute Myeloid Leukemia). Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida moja la utafiti wa kansa la Marekani lijulikanalo kama Journal of the American Association for Cancer Research.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!