MATUMIZI YA CHUMVI NA MADHARA YAKE
CHUMVI
• • • • • •
Mwili wa binadamu huhitaji madini ya sodium yanayopatikana kwenye chumvi ili kuwa na afya bora.Pamoja na umuhimu huu,matumizi mengi ya chumvi yanaweza kusababisha ukapata shinikizo la juu la damu (Presha).Unapotumia chumvi nyingi maana yake unaupa mwili wako madini mengi ya sodium zaidi ya inavyotakiwa.American Heart Assosiation wanashauri matumizi ya chumvi yasizidi kiasi cha wastani wa 1.5-2.3 gram kila siku.
Chumvi ikizidi sana mwilini huupa mwili kazi ya ziada ya kutunza maji mengi ili kuipunguzia nguvu.Jambo hili huongeza msukumo wa damu hivyo kusababisha mtu augue shinikizo la damu (presha).Unapokuwa na hali hii,magonjwa mengine nyemelezi yanakuwa na nafasi kubwa sana ya kukusumbua ambayo ni magonjwa ya moyo,kiharusi,kuacha kufanya kazi kwa moyo,kudhoofika kwa afya ya mifupa hivyo kuongeza hatari ya kuvunjika kutokana na kutolewa kwa madini ya calcium ili kufidia kiasi cha sodium kilichozidi,matatizo ya figo,saratani,kuongezeka kwa uzito na kupungua kwa uwezo wa ubongo hasa katika kutunza kumbukumbu,kufikiri,tabia na lugha.
Tumia chumvi ya kawaida tu kila siku,huna haja ya kutumia nyingi sana ili ujiepushe na magonjwa kama haya. Ni busara pia chumvi hii inapikwa moja kwa moja kwenye chakula ili kupunguza athari zake! cc.afyainfo
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!