🔻YAJUE MATUMIZI YA MAJANI YA KABEJI KWA WANAONYONYESHA
• • • • • •
MAJANI YA KABEJI KWA WANAO NYONYESHA: Kutokana na uwezo wake wa kupambana na mcharuko-mwili (inflammation), majani ya kabeji hutumiwa kwa kuwekwa juu ya matiti ili kupunguza maumivu/uvimbe utokanao na maambukizi katika matiti (mastitis). Pia hupunguza maziwa yanapojaa mno katika matiti (engorgement) na pia huweza kutumika kwa mama anaye muachisha nyonyo mwanae (weaning). Hatua za kuyatumia majani haya ni kama ifuatavyo;
1. Osha vizuri majani hayo na hakikisha yana ubaridi wa maji ama unaweza kuweka kwenye friji kidogo, kisha funika juu ya titi/matiti yako(sio lazima kuweka katika matiti yote kwa pamoja kama moja halina tatizo)
2. Hakikisha yamefunika titi vizuri, kisha unaweza tulia kwa kulala chali au kuyashikilia au kuvalia sindiria itakayoweza kuyashikilia vizuri ili majani hayo yasianguke
3. Pale tu majani hayo yanapoanza kutokuwa ya baridi ama zimefika dakika 20 tangu umeyaweka, basi YATOE
4. Tupa majani hayo, osha matiti yako vizuri kama utahitaji(kwani si lazima). Hakikisha hurudii kutumia majani yaleyale baadae
MUHIMU: Kama unatumia majani haya ili kupunguza maumivu, uvimbe au maziwa yamejaa basi Usiyaweke zaidi ya mara 3 kwa sababu kutumia zaidi huweza kusababisha upungufu kabisa wa maziwa ilhali bado unanyonyesha. ILA kama unatumia wakati unamuachisha mtoto nyonyo HAKUNA KIPIMO, TUMIA MARA NYINGI UWEZAVYO
Cr.drtareeq
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!