MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA HEDHI

 MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA HEDHI

➡️ Hedhi

Leo tutaangalia kuhusiana na maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.


Maumivu wakati wa hedhi ni ile hali mwanamke anajisikia maumivu ya tumbo (chini ya kitovu) wakati wa hedhi hali hii huwa inatokea mara nyingi kabla ya hedhi au huambatana na hedhi kwa pamoja.

.

Maumivu hayo mara nyingi huwa makali zaidi Pale ambapo yai linatoka kwenye ovari au linataka kutoka, na maumivu haya huweza kuwa makali zaidi hata kumsababishia mwanamke kushindwa kufanya kazi yoyote.

.

Uchunguzi unaonesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.

Sababu hizo ni kama  kuwa na umri wa chini ya miaka 20, kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo, kutoka  damu nyingi wakati wa hedhi, wanawake ambao hawajawahi kuzaa.

.

Kuna Magonjwa pia yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu zaidi ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:

 Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kutoka nje ya fuko hilo, au hata sehemu nyinginezo

Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaota katika mfuko wa uzazi.


PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga.

Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.

Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.

#hedhi #maumivu #tumbo #chiniyakitovu #mwanamke #afya #afyakwanza

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!