MAUMIVUYA TUMBO LA HEDHI (Dismenorrhea) NAMNA YA KUYAONDOA

HEDHI

• • • • • •

MAUMIVUYA TUMBO LAHEDHI (Dismenorrhea) NAMNA YA KUYAONDOA

Naumivu hayo hujitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni au wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.


Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani. Huanza pale tu yai linapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mrija wakati wa ovulation


AINA YA MAUMIVU

1: Maumivu yasiyokuwa na sababu zozote kimsingi na kitiba. Hutokea sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Huanza siku moja kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.


2: Maumivu yanayojumuisha na sababu nyinginezo za kitiba kama vile; matatizo ya kizazi, magonjwa wa nyonga na matatizo katika mirija ya mayai.


magonjwa ambayo husababisha maumivu wakati wa hedhi ni:-

ENDOMETRIOSIS

 ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kutoka nje ya fuko hilo au hata sehemu nyinginezo


ADENOMYOSIS ni uvimbe au tezi (tumors) ziotazo katika mfuko wa uzazi


PID ni maambukizi katika via vya uzazi 


Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi

Pia kuna baadhi ya magonjwa ambayo yanayoweza kusababisha mtu kupata maumivu ya tumbo la hedhi ni

Ugonjwa wa nyonga ambao mara nyingi husababishwa na bacteria watokanao na zinaa.


KUMBUKA

maumivu ya tumbo la hedhi hutegemeana na mtu na mtu. Mwingine anaweza pata dalili zote ma mwingine moja na mwingine baadhi tu au hata dalili moja. Wanawake wengi hujitambua tu bila msaada wa daktari.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!