🔻MFAHAMU FARAH KHALEK NA UGONJWA WA SCLERODERMA
• • • •
Farah Khalek ni mwanamke mwenye miaka 33 kutoka nchini Kenya.
Khalek ana ugonjwa wa ngozi unaojulikana kama Scleroderma.
Alizaliwa akiwa na sura kama ya mtoto mwenye muonekano wa kawaida.
Lakini alipofika umri wa miaka 17 hali yake ilianza kubadilika ambapo mikono yake ilianza kuwa migumu sana huku kucha zake zikibadilika rangi na kuwa bluu.
Mwili wa Farah umezidi kubadilika na kuchukua muonekano usiokuwa wa kawaida na binadamu wengine, ngozi nayo imeendelea kuwa ngumu na viungo vya mwili vimekuwa vigumu mno.
Baada ya uchunguzi ndipo alipogundua kuwa ana ugonjwa ambao hauna kinga unaojulikana kama 'scleroderma' .
Mwanamke huyu hawezi kufanya shuguli zake za kawaida kama kusimama , kuinama , kuandika kwa kalamu na kila mara anahitaji usaidizi wa mamake.
(Via bbcswahili)
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!