MGONJWA ATENGENEZA POMBE KWENYE KIBOFU CHAKE CHA MKOJO HIVO KUKOJOA POMBE

MAREKANI +MGONJWA+MKOJO+POMBE

• • • • • •

Siku kadhaa zilizopita watafiti katika mji wa Pittsburgh nchini marekani walilipoti mgonjwa wa kwanza kutengeneza pombe katika kibofu chake. 


Mwanamke huyu ambae ana umri wa miaka 61 ambae alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ini na kisukari alienda katika hospitali iliopo katika mji huo kwa ajili ya kupata utaratibu wa kupandikizwa ini baada ya ini lake kuharibika sana kwa kile ambacho awali waliamini ni kutokana na matumizi ya pombe kwa muda mrefu. 


Japo kuwa mwana mama huyo alikataa mara kadhaa kuwa hakuwa hakitumia pombe na hata hivyo hakuwa akionesha kabisa kuwa na dalili za ulevi. 


Walipofanya vipimo vya mkojo na damu waligundua kuwa katika mkojo kuna kiwango kikubwa sana cha pombe na kiwango kikubwa cha sukari.  Utafiti zaidi ulionesha kuwa fangasi "candida glabrata"  ambae hupatikana katika sehemu mbalimbali mwilini ndie aliekuwa akibadilisha ile sukari katika mkojo na kuichachusha na kuwa pombe. 


Jitihada zilifanyika na mwanamme huyo alipewa dawa za kutibu fangasi lakin haikuwa rahisi inawezekana ni kutokana na tatizo lake la kisukari. 


Watafiti waliuita huu ugonjwa "bladder fermentation syndrome"  walinukuliwa wakisema inawezekana wako wagonjwa wengi wenye tatizo hili ambao hawakugundulika.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!