Mimba Kutungwa Nje ya Mfuko wa Uzazi?( Ectopic Pregnancy)
Zaidi ya asilimia 95% ya mimba zinazotungwa nje ya mfuko wa uzazi huwa katika mirija ya fallopiani (Tubal pregnancies) na kwa asilimia zinazobakia mimba inaweza kutungwa sehem kama kwenye ovari na hata kwenye mlango wa uzazi (cervix).
VISABABISHI VYA MIMBA KUTUNGA NJE YA MFUKO WA UZAZI
-Uvimbe au maambukizi ndani ya mirija ya fallopiani yanayoweza kuzuia kiinitete kusafiri na kufika katika mfuko wa uzazi.
-Maambukizi ndani ya mfuko wa uzazi yanayo ondoa mazingira rafiki ya utungwaji wa mimba wa kawaida.
-Kovu lililobakia baada ya upasuaji, hasa ule wa mfumo wa uzazi linalosababisha kiinitete au yai kukwama na kushindwa kufika katika mfuko wa uzazi.
-Ukuaji usio wa kawaida(abnormal growth) na matatizo yanayojitokeza wakati wa kuzaliwa(birth defects) husababisha kuwepo kwa mirija ya fallopiani isiyo na umbo sahihi linalokwamisha usafirishaji wa yai au kiinitete hadi kwenye mfuko wa uzazi
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!