MJUE ANDREA BAINES MIONGONI MWA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA TATIZO LA ENDOMETRIOSIS
• • • • • •
Andrea Baines ni miongoni mwa mamilioni ya wanawake duniani wanaosumbuliwa na tatizo la Endometriosis.Yeye pamoja na mfanyakazi wake Rachel Berwick ambaye pia ni mgonjwa wa tatizo hili wameamua kwa pamoja kuja na ubunifu unaoonesha mateso,maumivu na usumbufu wanaoupata wanawake kutokana na uwepo wa ugonjwa huu ambao wanaeleza maumivu yake kama "Maumivu makali yasiyo na kipimo,yanayochoma kama sindano ya moto na kuleta usumbufu mkubwa wa viungo vya ndani ya mwili hali inayokuletea hisia ya kudhani kuwa vinanyofolewa kwa nguvu"
Kupitia kampuni yao ya @andreabainesmakeupartistry ,waliamua kutumia rangi za urembo wa asili kumpaka Rachel ili kulileta wazo hili kwenye uhalisia wa maisha ya watu katika kuonesha taabu na changanoto wanazopitia watu wenye tatizo hili.Kwa maana rahisi kabisa,Endometriosis ni tatizo linalotokea baada ya misuli,kuta au nyama zinazoshikilia mji wa uzazi zinapotengenezwa nje ya eneo hili mfano kwenye mirija ya uzazi,sehemu ya kutolea mayai ya uzazi,kwenye utumbo n.k.
Huambatana na maumivu makali sana ya tumbo wakati wa tendo la ndoa na hedhi,na miongoni mwa dalili zake zingine ni kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi,kupatwa na hedhi nzito sana pamoja na ugumba ikiwa halitashughulikiwa mapema.Matibabu yake makuu yapo katika makundi mawili ambayo ni matumizi ya aina mbalimbali za dawa pamoja na upasuaji kwa wale waliokawia sana kupata msaada wa matibabu! (Camera @ewilsonphotographer)
.
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!