MSONGO WA MAWAZO
🔻TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO
Tatizo hili hutokea kwa Watu wengi sana,huku wengine hata kufikia hatua ya kutoa uhai wao.
Zipo sababu Nyingi sana ambazo huweza kusababisha Msongo wa Mawazo,ikiwa ni pamoja na;
- Hali mbaya ya kiuchumi
- Migogoro mbalimbali ikiwemo ile ya mahusiano,Ndoa au Familia huchangia kwa Kiasi kikubwa Msongo wa Mawazo
- Mama Mjamzito,kupigwa,ugomvi,ujauzito kukataliwa n.k
- Kufanyiwa vitendo vya kikatili kama Kubakwa, n.k
- Kufukuzwa Kazi
- Kufiwa na mtu wa karibu kwako
- N.K...!!!
DALILI ZA MTU MWENYE TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO
- Kufanya kazi ndogo kwa Mda Mrefu,Mfano kufagia chumba kimoja,mtu huweza kufagia hata mpaka amalize saa zima.
- Kuanza kuongea mwenyewe pasipo na mtu wa kukusemesha
- Kuongea habari za kujiua au kumuua mtoto kwa wale waliojifungua
- Kuomba msamaha kila dakika hata kwa vitu ambavyo sio kosa
- Kupoteza kumbukumbu kwa gafla
KUMBUKA; endapo ukiona dalili hizi kwako au kwa mtu mwingine, mpeleke sehemu husika akapate tiba ya kisaikolojia na kuwekwa sawa kwani matokeo yake ni mabaya,Mtu huweza kufikia hatua ya Kujiua kabsa.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!