MSTARI MWEUSI KWENYE TUMBO WAKATI WA UJAUZITO NI NINI? NA HUSABABISHWA NA NINI?

MSTARI MWEUSI KWENYE TUMBO WAKATI WA UJAUZITO NI NINI? NA HUSABABISHWA NA NINI?

Viumbe Wote tuna mstari angalia picha ya mbele,ni CONNECTIVE TISSUE,inatoka kifuani mpaka kwenye mfupa wa nyonga,kila mtu anao,unaitwa LINEA ALBA.


Sema hauonekani sana.


Ila kipindi cha MIMBA,homon Za mimba zinafanya UZALISHAJI wa MELANIN,rangi nyeusi kuongezeka na kufanya chembechembe za rangi nyeusi kuongezeka mwilini na ndio maana unakuta wanawake wengi wanakuwa Weusi ziadi,lakin pia Sehemu za Maziwa kuzuguka chuchu na Kwenye mstari  huo wa tumbon hupata sanaaaa hizo chembechembe na kuwa nyeus sana.


Soma: Matumizi ya FLAGYL kuzuia mimba(ukweli wa mambo)


Unavyopinda au kunyooka ni maumbili tu ya mtu na jinsi  mtoto alivyokaa.


Wengine unakuwa mfupi wengine mrefu haina maana yeyote kitaalamu,muhimu stari UPO.


Wengi huanza onekana wiki ya 20 Hivi.


Kukolea au kutokukolea kwa mstari ni hali ya kawaida na mapokeo ya homon za mimba,ndio maana wengine wanatapika wengine hawatapiki.


Na mstari huu,HAUHUSIANI KABISA Na Jinsia za mtoto.

#Uzazipoint #afyaclass


Soma: Matumizi ya FLAGYL kuzuia mimba(ukweli wa mambo)


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!