MTOTO KUZALIWA NA MENO YA PLASTIKI (NATAL TEETH)

MTOTO KUZALIWA NA MENO YA PLASTIKI (NATAL TEETH)

➡️ Meno ya Plastiki

Haya ni meno ambayo mtoto huzaliwa nayo,mara nyingi hua ni meno mawili ya chini(mandibula incissors). Hali hii sio ya kawaida kutokea kwa jamii lakini hua inawatokea baadhi ya Watoto. Kitakwimu kati ya Watoto 10000-20000 wanaozaliwa mmoja wao anakua na meno ya plastiki.


Kwa kweli kinachosababisha baadhi ya Watoto wazaliwe na meno ya plastiki bado hakijulikani vizuri lakini ziko baadhi ya tafiti zinaelezea uwepo wa sababu za kijenetiki  kwenye jambo hili na pia uvutaji au utumiaji wa kemikali chafuzi za kimazingira kwa mama mjamzito kama polychlorinated biphenyls (PCBs), dibenzofurans (PCDFs) na  polychlorinated dibenzo-p-dioxins (PCDDs. Kemikali hizi zinaweza kupita kwenye mpaka wa kondo la nyuma na mzunguko wa mama(have the capacity to cross the placenta),vile vile kemikali hizi zimepatikana pia kwenye maziwa ya mama(have also been detected in the milk of the mother).


Hali hii imekua ikihusishwa na imani za kishirikina si afrika tu bali hata barani asia na ulaya,mfano kwa afrika inasemwa kwamba kama mtoto amezaliwa na meno ni mkosi na balaa kwa familia na ukoo mzima,nchini uingereza na ufaransa mtoto akizaliwa na meno huchukuliwa kama ishara ya ushindi na kama mtu atakaekuja kuteka dunia nzima,kule India/Poland/china mtoto anaezaliwa na meno ni mkosi na akimg’ata mzazi mmoja basi atafariki…jamani hizi ni Imani tu na hazina uhusiano wowote juu ya mambo haya ya kisayansi.


Mtoto akizaliwa na meno basi wazazi hufahamishwa na taratibu za kimatibabu(kama kuyang’oa) hufanyika kwa kuwashrikisha wazazi


Mojawapo ya madhara ya hatari ni jino kutoka na kuingia kwenye mapafu na kumletea mtoto shida ya kupumua hata kufa


watu kama Julius kaisari na Napoleon walizaliwa wakiwa na meno🙌


USHAWAHI KUONA MTOTO ALIEZALIWA NA MENO??ULIWAZA NINI ULIPOONA?

.

#Dr.Mathew #afyaclass

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!