MTOTO WA JICHO
• • • • • •
Hali ya Mtoto wa Jicho inatokea pale lenzi ya jicho inapopata ukungu na kuathiri uwezo wa kuona. Mtoto wa jicho ndio chanzo kikuu cha upofu kwa watu wenye miaka zaidi ya 40.
CHANZO
Sababu kubwa ya Mtoto wa Jicho ni umri mkubwa. Kama una umri zaidi ya miaka 40 na unaona hali ya ukungu katika jicho lako basi unaweza kuwa na mtoto wa jicho. Pia mtoto wa jicho inaweza kusababishwa na: ugonjwa wa kisukari, presha ya damu, ajali katika jicho au kukaa muda mrefu kwenye jua kali.
DALILI
Huwa hakuna dalili katika hatua za mwanzo za mtoto wa jicho. Baadaye mtu mwenye mtoto wa jicho huwa anaona ukungu, haoni vizuri nyakati za usiku, pia huwa anasumbuliwa sana na mwanga.
KINGA
Ulaji mzuri wa mboga, matunda na vyakula vyenye antioxidant unapunguza uwezekano wa kutokea mtoto wa jicho kwa watu wenye umri mkubwa. Pia uvaaji miwani ya jua unasaidia macho kutopatwa na mtoto wa jicho.
TIBA
Hali ya mtoto wa jicho inaweza kutibika kwa kuondoa lenzi yenye ukungu kwa njia ya upasuaji. Ni upasuaji mdogo chini ya dakika 30 ambapo mgojwa anaruhusiwa kurudi nyumbani siku hiyo hiyo.
#afyabongo #drtareeq
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!