MVINYO
• • • • • •
MVINYO MWEKUNDU
Karne kadhaa zilizopita,mvinyo mwekundu ulitumika kutatua changamoto kadhaa za kiafya.Watawa wa Medieval waliamini kuwa makasisi wao waliishi miaka mingi kuliko watu wengine kutokana na unywaji wa kiasi wa mvinyo kila siku wanapokuwa wanaadhimisha sadaka za misa takatifu kwa mujibu wa utaratibu wa kanisa la Roma.
Mvinyo mwekundu umekuwa pia unasomwa kwa miaka mingi sana na baadhi ya ripoti na tafiti mbalimbali zinautaja kuwa na faida za kurefusha muda wa kuishi kwa kukukinga dhidi ya magonjwa hatarishi,hutoa kinga dhidi ya aina mbalimbali za saratani,huboresha afya ya ubongo na moyo,huimarisha mfumo wa usafirishwaji wa damu mwilini pamoja na kuongeza ufanisi wa homoni za Insulin katika kudhibiti ongezeko la sukari mwilini.
Mvinyo huu huwa na kemikali muhimu za Resveratrol ambazo hupatikana pia kwenye matunda ya mzabibu hivyo yanaweza pia kutumika moja kwa moja kama mbadala wa mvinyo.Hata hivyo,kwa usalama wa afya ya mtumiaji,hushauriwa mwanamke asitumie zaidi ya glasi moja kila siku huku mwanamme akishauriwa asitumie zaidi ya glasi 2 kila siku.Matumizi yaliyozidi husababisha utegemezi,kiharusi,shinikizo la juu la damu,sonona,matatizo ya moyo,pia Ini na figo.
Wanawake wajawazito na wanaonyonyesha,wagonjwa wa pumu,Gout,vidonda vya tumbo,kiungulia,matatizo ya akili na wale wenye matatizo ya Ini na figo hawapaswi kutumia kinywaji hiki.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!