MWANAMKE KUPATA PERIOD MARA MBILI AU ZAIDI NDANI YA MWEZI MMOJA SABABU NI HIZI

PERIOD

• • • • • •

MWANAMKE KUPATA PERIOD MARA MBILI AU ZAIDI NDANI YA MWEZI MMOJA SABABU NI  HIZI.


Kwa Wanawake wengi mzunguko wa hedhi huwa ni wa siku 28. Ingawa wengine huwa na mizunguko kuanzia siku 21 hadi 35.


Kupata hedhi mara mbili kwa mwezi kunaweza kutokea iwapo siku hizo za mzunguko zitakamilika katika mwezi mmoja.

Kwa mfano, iwapo msichana anapata hedhi tarehe 1 mwezi wa saba, kama mzunguko wake ni siku 26 msichana huyu atapata tena hedhi katika tarehe 27 ya mwezi wa saba.


Hivyo atakuwa amepata hedhi mara mbili katika mwezi mmoja. Vilevile, inatokea kwamba mwanamke anapata hedhi katikati ya mzunguko wake ( kwa mfano, baada ya siku 14 katika mzunguko wa siku 28 ). 


Zipo sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mwanamke akarudia hedhi katika mwezi. Sababu hizi ni kama


1.mabadiliko ya hali ya hewa au mazingira. 

2.uvimbe katika kizazi( uterine fibroid)

3.matumizi ya uzazi wa mpango

4.Hormone kutobalance

5.kufanya mazoezi kupita kiasi

Ikumbukwe ni vigumu mwanamke kubeba ujauzito kama period yake inabadilika badilika

.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!