NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUINGIWA NA MDUDU SIKIONI
NINI CHA KUFANYA?
1. Elekeza kichwa chako kuelekea juani. Kama ni gizani/usiku elekeza kwenye chanzo cha mwanga kama taa/tochi. Mdudu huweza kufuata mwanga na kutoka sikioni
2. Chukua kipande kidogo cha tufaha(apple) kiweke jirani na sikio lako. Mdudu huvutiwa na harufu yake na huweza kutoka nje
3. Mdudu aingiapo sikioni huweza kunasa katika nta(earwax) au huweza kudhoofika/kuishiwa nguvu ya kutoka nje hivyo,
Inamisha kichwa upande kwa chini na mtu mwingine akutie mafuta ya zaituni(olive oil) ama mafuta mengine yatokanayo na mimea (vegetable oil) au baby oil kwenye sikio lenye mdudu.
Mafuta yenye uvuguvugu(sio ya moto) hufaa zaidi. Mafuta yakisha ingia ruhusu yakae kwa muda wa dakika moja hivi halafu ruhusu yatoke kwa kuinamisha sikio yanapotoka hutoka na mdudu.
Unapoinamisha sikio livute nyuma kwa juu ili kuruhusu njia (ear canal) kwa mdudu kutoka.
4. Kama hakuna ahueni, Weka maji ya uvuguvugu(sio ya moto) sikioni ukiwa umeinama na kulivuta sikio nyuma juu. Mdudu huweza kutolewa pamoja na maji hayo
MUHIMU: Kama haya yote hayajafanikisha kumtoa mdudu, Fika Hospitali!
MAMBO YAPI HUPASWI KUFANYA?
1. Usitumie vijiti vya pamba kumtolea mdudu
2. Usiingize vijiti vya meno au vya kibiriti kumtolea mdudu
3. Usiingize kidole chako sikioni, Kwani mara nyingi humsokomeza mdudu ndani zaidi
4. Usitumie maji ama mafuta ya moto sana
5. Kama una maumivu makali au kuvuja damu sikioni usifanye lolote bali wahi hospitali .
MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA
1. Maumivu makali ya sikio
2. Kupoteza usikivu
3. Kuvuja damu sikioni
4. Maambukizi (infection)
5. Kutoboka kwa ngoma ya sikio (eardrum)
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!