NJIA NANE (8) ZA KUBORESHA UWEZO WA UBONGO WAKO

NJIA NANE (8) ZA KUBORESHA UWEZO WA UBONGO WAKO

Mara nyingi tunaambiwa kuwa uwezo wa kukumbuka unapungua wakati mtu anazidi kuwa mzee


Lakini kuna matumaini kuwa kuna njia za kuboresha ubongo wetu.


Kwa hivyo kama unataka kuboresha uwezo wa ubongo wako basi kuwa tayari kufanya mambo haya.


1.Mazoezi hufanya ubongo wako kuwa mkubwa


Mazoezi huchangia ubongo kuwa na mawasiliano mazuri na pia huchangia seli zaidi kukua.


Kama unafanyia mazoezi yako nje basi inakuwa bora kwa sababu utakuwa na manufaa zaidi ya kupata vitamini D


2.Kariri vitu ukiendelea na shughuli zingine.

Hii ni mbinu ambayo pia imetumiwa na wacheza filamu: kama unajaribu kukariri maneno fulani au kujaribu kujifunza kitu huku ukitembea tembea, unaweza kushika kwa njia rahisi kile unachokariri


3.Kula chakula kinachosaidia kukua kwa ubongo.

Karibu asilimia 20 ya sukari au chakula cha kutupa nguvu unachokula kinaelekea kwa ubongo, na kuufanya ubongo kutegemea sana sukari.


Seli za ubongo hujengwa kwa mafuta, kwa hivyo ni muhimu kutotoa mafuta kutoka kwa chakula chako. Mafuta kutoka kwa njugu, nafaka , parachichi na samaki ni muhimu kwa afya ya ubongo.


4.Kupumzika

Misongo mingine ya mawazo ni muhimu kwa sabubu inatuwezesha kuchukua hatua za haraka wakati wa dharura.


Lakini msongo wa muda mrefu huathiri sana ubongo. Hivi basi tunastaili kupumzisha ubongo.


5.Tafuta njia zingine za kujipa changamoto.


Njia muhimu ya kuboresha ubongo wako ni kuwa na changamoto kwa kujifunza kitu kipya kabisa.


Shughuli kwa mfano kujifunza kuchora au kujifunza lugha mpya huchangia ubongo kuboreka zaidi.


Unaweza pia kucheza michezo ya mitandaoni dhidi ya marafiki au watu wa familia.


6.Sikiliza Muziki.

Ushahidi unaonyesha kuwa muziki huboresha ubongo kwa njia ya kipekee


Wakati ukiangalia ubongo wa mtu ambaye anasikiliza muziki au anayecheza muziki ni kuwa ubongo wote hushiriki.


7.Somea mtihani kitandani

Kama utajifunza kitu kipya wakati wa mchana, huwa kunatokea mawasiliano kati ya seli moja ya ubongo na nyingine


Unapolala, mawasiliano huwa dhabiti na huwa unakumbuka kile umejifunza.


Ikiwa unasomea mtihani, jaribu kupitia maswali na majibu kichwani mwako wakati unakaribia kulala.


8.Amka vizuri


Itaendelea....

Na. @DR.Ngimi

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!