PAPAI
• • • • • •
PAPAI NA FAIDA ZAKE KIAFYA.
Asili ya mpapai ni Amerika ya kati, ambapo kuanzia matunda,majani na utomvu wa mmea huu hutumiwa kama dawa maeneo mbalimbali duniani.
Vilevile matunda na utomvu wake yamekuwa yakitumika kutengeneza pombe na mvinyo katika baadhi ya nchi,huku wengine wakitumia mpapai kama dawa kwa mifugo na binadamu.
Wataalamu wa lishe wanaeleza kuwa wenye matatizo ya kupatwa na majipu ,uvimbe na vidonda Mara kwa Mara huwa na upungufu wa virutibisho muhimu ambavyo huweza kupatikana ndani ya papai,hivyo imegundulika watu wenye matatizo hayo wakitumia papai hupata nafuu na kupona haraka.
Pia papai husaidia kuleta nuru ya macho,kama inavyoaminika kwa karoti papai pia husaidia kupunguza madhara yatokanayo na moshi wa sigara. Hivyo wavutaji wa sigara ni vyema watumie papai kwa wingi ili kujipunguzia madhara ya moshi wa sigara.
Ni wazi kuwa papai lina utajiri wa vitamini kuliko matunda mengine kwani lina vitamin A,B,C,D na E.
Tunda la papai lina faida nyingi kwa afya ya binadamu.miongoni mwa faida hizo ni ;
>Kutibu tatizo la shida ya kusaga chakula tumboni.
>Kutibu udhaifu wa tumbo.
>Kutibu kisukari na asthma au pumu.
>Kutibu kikohozi kitokacho mapafuni.
>Kutibu kifua kikuu
>Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku.
>Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda NA sehemu palipoungua moto.
MBEGU:Mbegu zake hutibu homa.meza mbegu za papai kijiko cha chakula Mara 3.
-Mbegu za papai zilizokaushwa ndani kisha kusagwa kuwa unga zinatibu malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji,kunywa Mara 3 kwa siku 5.
MIZIZI:mizizi ya papai ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa ,lita2 na nusu kwa dak 15,yanatibu figo,bladder na kuzuia kutapika. Nusu kikombe cha chai kutwa Mara 3 siku 5.
Prepared by Dr Sam CEO/ founder of SAM NUTRITIONAL CLINIC
.
.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!