PARACETAMOL KUATHIRI UWEZO WA KUZALISHA

PARACETAMOL

• • • • • •

Utafiti wa Wanasayansi nchini Uingereza umebaini kuwa unywaji wa dawa zenye kiungo cha Paracetamol kwa kipindi cha siku saba unapunguza uwezo wa uzalishaji wa homoni za kiume ''testosterone''. Homoni hiyo ndio inayowezesha kuumbwa kwa sehemu ya uzazi wa kiume.


Sasa madaktari wanashauriwa wasipeane dawa zenye ''Paracetamol'' kwa wanawake waja wazito kiholela. Na iwapo itawalazimu kupeana dawa hizo basi wanashauriwa kupeana dawa hizo kwa kipindi kifupi ilikupunguza madhara kwa watoto waliotumboni.


Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa onyo kutolewa dhidi ya wanawake wajawazito kupewa dawa zilizo na kiungo cha Paracetamol. Awali utafiti wa wanawake wajawazito 2,000, nchini Denmark ulibaini kuwa,wanawake waliomeza dawa za Paracetamol walijifungua watoto waliolemaa katika sehemu ya mfuko wa uzazi- korodani


Ulemavu huo hatimaye ulijitokeza na kuwa upungufu wa uwezo wao kuzalisha katika maisha yao ya utu uzima.


Aidha inasemekana kuwa wanawake wanaotumia dawa hiyo ya kupunguza maumivu kwa kipindi kirefu wakati wa ujauzito, wanaweza kuathiri mimba zao na hasa kwa watoto wavulana.


Wanasayansi hao wa Chuo kikuu cha Edinburgh, walitumia panya katika utafiti huo.


Shirika linalosimamia maswala ya afya Nchini Uingereza, linasema kuwa wanawake waja wazito wanafaa kumeza tembe hiyo ya paracetamol ikiwa tu wameshauriwa na daktari na pia kwa kipindi kifupi mno.


Dakta Rod Mitchell, aliyeongoza utafiti huo anasema kuwa tahadhari kubwa inapaswa kuwekwa inapowadia swala la matumizi ya Paracetamol miongoni mwa wanawake waja wazito.


Licha ya utafiti huu msemaji wa chuo cha afya ya watoto nchini Uingereza Dr Martin Ward-Platt, anaonya kuwa wanadamu hawapaswi kukatazwa kabisa kumeza dawa zilizo na Paracetamol kwa sababu zinasaidia sana kutibu na wakati mwingine Paracetamol hutosha kutibu homa.


Daktari Sadaf Ghaem-Maghami, kwa upande wake ameonya kuwa utafiti huo haupaswi kukubalika pasi na maswali muhimu kuulizwa kuhusu ukweli wake. ''Licha ya kuwa matokeo ya utafiti huu ni mazuri ,tunapaswa kufanya utafiti zaidi kwa sababu utafiti huu ulifanyiwa wanyama, Je mwili wa binadamu utaitikia vipimo vya dawa hii kwa njia sawa na hiyo? alihoji dakta Sadaf.

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!