RANGI ZA MKOJO PAMOJA NA MAANA ZAKE KIAFYA KATIKA MWILI WA BINADAMU

ZIJUE RANGI ZA MKOJO PAMOJA NA MAANA ZAKE KIAFYA KATIKA MWILI WA BINADAMU

• • • • • •

Mwili wa binadamu ni kama mashine,unapopatwa na tatizo lolote huwa hauachi kufanya kazi moja kwa moja ila hutoa aina fulani za viashiria kukupa taarifa juu ya uwepo wa tatizo hilo.Mojawapo ya vitu vinavyotoa ishara ya uwepo wa tatizo mwilini ni mkojo kupitia rangi zake tofauti

-

1)NJANO MPAUKO/DHAHABU.

Inaonesha kila kitu kiko sawa mwilini.Rangi hii husababishwa na chembechembe za urochrome zinazozalishwa na mwili

-

2)HAKUNA RANGI(kwa uelewa tusema mweupe)

Inaonesha umetumia kiasi kikubwa cha vimiminika au maji.Inawezekana pia umetumia vyakula/dawa/vinywaji aina ya diuretic (vitu vinavyosababisha mwili utoe maji mengi kupitia mkojo). Ni sawa

-

3)ASALI MBICHI/KAHAWIA.

Inaonesha unakabiliwa na upungufu mkubwa wa maji (dehydration) hivyo ongeza unywaji wa maji.Inaweza kumaanisha pia kuna tatizo katika ini hivyo isipoisha ndani ya siku 2 au 3 baada ya kunywa maji mengi basi fika hospitalini

-

4)PINKI/NYEKUNDU.

Inasababishwa na ulaji mwingi wa vyakula kama blackberries na karoti.Pia hutokea baada ya kunywa dawa za antibiotics (kama rifampin na phenazopyridine) hasa wakati wa kutibu magonjwa kama UTI.Wakati mwingine damu pia inaweza kuwemo,hii haimaanishi moja kwa moja kuwa ni tatizo lakini mara nyingi humaanisha tatizo la figo,uvimbe,UTI au tezi dume.Muone daktari

-

5)RANGI YA CHUNGWA.

Kutokana na muonekano wake inaweza kumaanisha upungufu wa maji mwilini(dehydration),ini au nyongo hivyo pata usaizidi wa matibabu haraka.Pia inaweza kutokea baada ya kunywa dawa kama phenazopyridine,dozi ya vitamin B2

-

6)BLUU/KIJANI.

Hali hii hutokea baada ya kula vyakula vilivyo wekewa rangi hizi au dawa kama anesthetic propofol (dawa ya kuondoa maumivu) na promethazine (dawa ya allergy/asthma).Rangi hii pia ikiendelea kuwepo kwa siku 2 au 3 pata msaada katika kituo cha afya kilicho karibu yako

-

7)MUONEKANO WA POVU LA SABUNI.

Mara nyingi humaanisha uwepo wa protini nyingi kwenye figo jambo ambalo siyo zuri sana kwa afya yako.Tafuta tiba.

-

Mkojo ni kiashiria muhimu sana katika kutoa mrejesho wa jinsi usawa wa mwili na afya zetu ulivyo hivyo tunapoona mabadiliko yasiyo ya kawaida ya rangi ya mkojo ni vema kutokupuuzia.Tutafute msaada wa tiba na ushauri mapema.cc.afyainfo

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!