MIGUU KUVIMBA
• • • • • •
SABABU YA KUVIMBA MIGUU UKIWA SAFARINI NA MATIBABU YAKE
Kuna watu wengi hupatwa na hii hali ya kuvimba miguu pale wanaposafiri hususani umbali Mrefu. Safari ambayo huhusisha kukaa kwa Mda mrefu kwenye kiti cha Gari. Ingawaje sio lazima ukiwa tu unasafiri, ila kuna wengine hata akikaa mda mrefu akiwa nyumbani Miguu huvimba.
JE NINI KINASABABISHA HALI HII?
Kwa kitaalam hali hii hutokana na kukosekana kwa Mzunguko wa Damu mzuri katika mishipa ya miguu kutokana na kukaaa kwa mda mrefu, hivo kupelekea damu kutuwama sehemu moja na kupelekea Maji yaliyopo ndani ya mishipa Ya damu kutoka na kujikusanya kwa Nje hivo kutengeneza hali ya Uvimbe kwenye miguu
MATIBABU
Kuvimba miguu ukiwa safarini sio tatizo, hali hii huweza kuisha yenyewe ndani ya mda mfupi baada ya wewe kutoka ulipo kaa na kuanza kutembea,Ila endapo kuvimba huko kumekaa kwa mda mrefu hata baada ya kutembea, huku ukiendelea kupata maumivu makali basi huenda kuna shida nyingine kama Damu kuganda N.K hivo ni vizuri kuongea na wataalam wa afya kujua nini shida
MAMBO YA KUFANYA;
1. Anza kutembea baada ya kuona shida hii ya kuvimba miguu
2. Epuka kuvaa viatu vinavyobana miguu
3. Endapo maumivu na uvimbe bado upo,waone wataalam wa afya
Kwa Ushauri zaidi,Elimu au Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!