SABABU ZA KUVUJA DAMU WAKATI WA UJAUZITO

➡️ ZIJUE SABABU ZA KUVUJA DAMU WAKATI WA UJAUZITO


Naifahamike kwamba,Moja ya Dalili za Hatari Kwa Mjamzito ni Kuvuja damu ukiwa Mjamzito; Zipo sababu Mbali mbali ambazo huchangia Tatizo hili ambazo ni Pamoja na;


1. Kondo la Nyuma kushuka na kujishikisha kwa chini karibu na Mlango wa uzazi kitaalam hujulikana kama Placenta praevia


2. Kondo la Nyuma kuachia kabsa kutoka sehemu lilipojishikiza kitaalam hujulikana kama Placenta abruption


3. Mjamzito kupatwa na tatizo la Damu kushindwa kuganda kitaalam hujulikana kama Coagulopathy


4. Kupata mshuto wa mimba na majeraha kutokana na sababu mbali mbali kama vile kuanguka,kupigwa n.k


5. Kupatwa na tatizo la Kupasuka kizazi yaani Rupture of Uterus


6. Kupata majeraha kwenye mlango wa uzazi


7. Kupata Majeraha sehemu za siri au ukeni


8. Kupatwa na Kansa ya kizazi au shingo ya kizazi


MATOKEO


- Damu kuvuja

- Maumivu ya tumbo,mgongo na tumbo kukaza sana na kuwa gumu

- Hali ya mtoto tumboni kuanza kubadilika yaani Fetal distress

- Kuanza kupata uchungu wa kuzaa kabla ya wakati yaani Premature labor

- Mtoto kufia tumboni.

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!