SABABU ZA KUZAA MTOTO MKUBWA(BIG BABY)
🔴 SABABU ZA KUZAA MTOTO MKUBWA(BIG BABY)
Mtoto anapozaliwa na Kilo zaid ya 3.5 ni Mtoto mkubwa,kitaalamu tunaita BIG BABY.
Kilo za kawaida ambazo mtoto hupasawa kuzaliwa nazo ni kilo 2.5 mpaka kilo 3.5,zaidi ya Hapo ni mtoto mkubwa au kwa kitaamu Big baby
ZIPI NI SABABU ZA MTOTO KUZALIWA MKUBWA?
Visababishi vya mtoto kuwa Mkubwa ni pamoja na;
1.Mama anapokuwa na kisukari, hii inafanya watoto kuzaliwa na kilo nyingi sana
2.Mama anapokuwa ananenepa sana wakati wa ujauzito kutokana na Ulaji wa mara kwa mara,ile kula kula kwa mimba,haswaaa ulaji wa chips na mayai yake,wengi wanajifungua watoto vibonge ivi...
3.historia ya wazazi , kama wana asili ya Ubonge basi chance ya mtoto kuwa bonge ni kubwa pia...
Mara nyingi Mimba ya kwanza,mtoto akiwa na Kilo kuanzia 4(baada ya kupigwa ultrasound),wengi huwa tunashauri moja kwa moja afanyiwe upasuaji.....mtoto anavyokuwa mkubwa,uwezekano wa kukwama na kushindwa kutoka kwa njia ya kawaida ni mkubwa,hivyo kuweka maisha ya mtoto na ya mama kuwa hatarini.
Je wewe Ulizaliwa na Kilo Ngapi? au Umezaa mtoto wako wa kwanza na Kilo Ngapi?
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!