FAHAMU
• • • • • •
SABABU ZA MUWASHO MWILINI
Miongoni mwa sababu za kutokea kwa muwasho wa mwili baada ya kuoga ni za kimazingira na sababu zingine zinahusiana na hitilafu za urithi wa vinasaba vya kijenetiki katika mfumo wa kinga ya mwili wa mhusika.
Wakati mwingine tatizo hili linaweza kuwa ni dalili muhimu inayoonyesha baadhi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kama vile matatizo ya
Figo, ini, tezi shingo, matatizo ya mfumo wa damu, kisukari, saratani ya mitoki na msongo wa mawazo.
Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwa sababu nyingine ni pamoja na uchafuzi wa mazingira ya hewa kwa kemikali zenye sumu zinazopatikana katika moshi wa tumbaku, mifuko ya plastiki, dawa za kufanyia usafi majumbani, dawa za kuua wadudu, vumbi ya ndani ya nyumba yanayobeba vimelea vya magonjwa pamoja na uchafuzi wa hewa kwa moshi wa magari na ule unaozalishwa na viwanda katika maeneo ya mijini.
Vitu hivi huufanya mwili kuathirika na kutengeneza mazingira ya ndani ambayo yanachochea kutokea kwa muwasho pindi mwili unapopata msisimuko, hali ambayo hujulikana kama mzio.
NI KWA NAMNA GANI?
Baadhi ya watafiti wanabainisha kuwa kutokana na hitilafu za vinasaba vya kijenetiki kunakuwa na ongezeko la kemikali aina ya Cyclic Adenosine Monophosphate Phosphodiesterase ambayo inaharibu mfumo wa udhibiti wa seli za kinga mwili aina ya basophils na seli za mast na kusababisha zisisimuke kupita kiasi na kuzalisha histamine nyingi ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa mzio.
Watu wengi wana mzio wa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na dawa za tiba, kemikali zinazotumika kutengenezea sabuni, vipodozi, aina fulani za vyakula, kemikali kadhaa zinazotumika katika usindikaji wa vyakula, kemikali zinazowekwa katika maji kama vile chlorine (watergurd), maji ya kuoga yenye chumvi nyingi na kemikali zinazotumika katika utengenezaji wa nguo, ikiwa ni pamoja na mataulo ya kuogea.
Mapambano kati ya kinga mwili na kile ambacho mwili hukibainisha kwa makosa kama wavamizi, yanaweza kusababisha magonjwa ya pumu, muwasho wa ngozi, muwasho wa macho, mafua ya mara kwa mara na maumivu ya tumbo.
itaendelea......................
.
#Healthchecktz
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!