SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA HEDHI

HEDHI

• • • • • •

SABABU ZA KUKOSA HEDHI.


Visababishi vya mwanamke kukosa hedhi vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu,


 • Vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni,


 • Vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi ya mwanamke.


•Vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke.


Leo tutaangalia matatizo katika ovari yanavyopelekea tatizo la kukosa hedhi.

Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike yaani ovari ni pamoja na:

➢ Kutozalishwa kabisa kwa mayai.

➢ Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu.

➢ Kuvimba kwa ovari hupekekea ovari kushindwa kufanya kazi yake vizuri.

➢ Ovary kuwa na vifukovifuko (POS) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa.

➢ Kufa na kushindwa kufanya kazi kwa ovari kabla ya muda wake.

➢ Ukosefu wa kimaumbile wa ovari ambao hutokea wakati wa ukuaji.

➢ Kufa kwa ovari baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili.

➢ Historia ya kuwahi kupata tiba ya mionzi au madawa yanaathiri ovary.


Dalili za kukosa hedhi.


Ikumbukwe kukosa hedhi siyo ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo kwa tatizo au ugonjwa fulani katika mwili. Kulingana na ugonjwa unaosababisha tatizo hili, kukosa hedhi kunaweza kuambatana pia na:


1. Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito na wala hanyonyeshi, maumivu ya kichwa na matatizo katika kuona vitu ambavyo kwa pamoja vinaweza kuashiria uwepo wa uvimbe katika ubongo.


2. Mwanamke kuwa na nywele na vinyweleo vingi mwilini na kuota ndevu kama mwanaume hali inayoashiria kuwepo kwa wingi kwa homoni za kiume za androgen.


3. Ukavu katika uke, kutoka jasho sana wakati wa usiku, au mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria matatizo katika ovari.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!