MIMBA
• • • • • •
SABABU ZA MWANAMKE KUTOKUSHIKA MIMBA (INFERTILITY)
Kwa kawaida mwanamke anatakiwa apate ujauzito ndani ya mwaka mmoja baada tu ya kuolewa au kuanza uhusiano. Tunategemea baada ya miaka miwili hadi mitatu baada ya kupata mtoto apate mwingine labda kama hajaamua yeye pamoja na mumewe. Ujauzito unapatikana baada ya kufanya tendo la ndoa kwa ukamilifu, yaani katika kipindi ambacho mwanamke anaweza kupata ujauzito (siku za hatari).
Swala hili pia linaangalia kwa upande wa pili wa mwanaume ambaye pia tunategemea ana uwezo huo wa kumpa mwanamke mimba kwa kuwa na mbegu zenye ubora na nyingi, pia awe na nguvu za kutosha za kufanya tendo ili mwezi wake apate ujauzito. (Kuhusu mwanaume tayari somo lake).
ZIPO AINA MBILI ZA KUTOSHIKA MIMBA (INFERTILITY)
1. AINA YA KWANZA (PRIMARY INFERTILITY)
Hii ni kwa wale ambao mke na mume hawakuwai kubahatika kupata mtoto hata mmoja tangu waoane au wawe kwenye mahusiano ili hali wanakutana kimwili bila kutumia kinga yoyote Ile.
2. AINA YA PILI (SECONDARY INFERTILITY)
Hii ni kwa wale ambao mke na mume walishazaa mara moja Lakini hawafanikiwi kupata mtoto mwingine ili hali wanakutana kimwili bila kutumia kinga yoyote.
Vitu vinavyosababisha mwanamke kushindwa kupata mimba ni:-
1.Kutokuwa na uwiano mzuri wa homoni (Hormonal Imbalance)
2.Ovaries kushindwa kutoa mayai
3.Kuziba kwa mirija ya uzazi
4.Mirija ya uzazi kujaa maji
5.Uvimbe katika kizazi (uterine fibroid)
6. Magonjwa kama vile PID, kisonono kisukari nk
7.Kuwa na msongo wa mawazo
8.Utoaji wa mimba (Abortion)
9.kuwa na uzito kupita kiasi (over-weight)
10.Matumizi ya pombe, bangi, sigara, ulevi kupindukia
11.Matumizi ya madawa
12.Endometriosis:-Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuota nje ya fuko hilo au hata sehemu nyingine.
Hizo hapo ni baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha mwanamke asipate ujauzito.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!