Ticker

6/recent/ticker-posts

SAHANI YA MLO KAMILI INAVYOTAKIWA KUWA(BALANCE DIET)



MLO KAMILI

• • • • • •

Lishe na namna tunavyokula ndio msingi mkuu wa kupungua au kuongezeka uzito.


SAHANI YA AFYA ( HEALTHY PLATE) ni mpangilio maalum wa lishe uliothibitishwa na shirika la afya duniani. Mpangilio wa lishe kulingana na makundi ya chakula ni kama ifuatavyo:


1. Kwa kila mlo MATUNDA NA MBOGA za majani yajaze nusu (1/2) ya sahani yako ya chakua


Chagua matunda na mbogamboga aina zaidi ya moja yenye rangi tofauti tofauti; kila rangi husadifu faida fulani kiafya. Mboga hukupa virutubisho bila kukufanya uwe mnene.


2. Vyakula vya PROTINI vichukue robo (1/4) ya sahani


Unatakiwa kuchagua protini zinazotokana na mimea kama maharage, soya, njegere, karanga. Lakini pia unaweza tumia mayai, samaki, kuku.


Punguza kutumia nyama nyekundu na kama huwezi kujizuia basi usizidi nusu kilo kwa wiki.


3 NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA kama dona, ulezi, mtama, mchele wa brown, mkate wa brown zichukue robo (1/4) tu ya sahani


Nafaka zisizokobolewa zina nyuzi lishe nyingi na hukufanya usile sana, pia hazisababishi sukari nyingi kwenye damu hivyo kuzuia mtu asinenepe.


4. MAFUTA SALAMA YA KUPIKIA

Chagua mafuta salama kiafya ya kupikia kama mafuta ya olive, soya, karanga na alizeti.


Epuka mafuta ya wanyama au mafuta yanayoganda yakipoa.


5. Kunywa MAJI ya kutosha

Epuka vinywaji vyenye sukari kama soda, pombe. Tumia juisi kiasi kama ukinywa iwe glasi moja kwa siku 


MUHIMU: Huu ni muhtasari wa muongozo wa sahani lishe (health plate): Kula zaidi asubuhi, kula kidogo usiku. Usitegemee matokeo ya haraka, ukijikondesha haraka,utanenepa tena #drtareeq

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!






Post a Comment

0 Comments