TABIA YA KULA UDONGO WAKATI WA UJAUZITO

KULA UDONGO WAKATI WA UJAUZITO

• • • • • •

Pica ni mjumuisho wa tabia za ulaji wa vitu visivyo vyakula. Hali hii inaweza kumpata mtu yeyote yule,lakini kwa upekee kabisa tujaribu kuona mojawapo ya aina za “Pica” inayotokea kwa wanawake wajawazito ambayo ni ulaji wa udongo/mchanga. Hali hii hutoa maana kubwa ya uwepo wa upungufu wa virutubisho muhimu pamoja na uchache wa madini ya chuma

-

Tabia hii inaweza kusababisha kutokea kwa tatizo la choo kigumu,kuziba kwa utumbo,kuzaliana kwa minyoo kwenye tumbo na utumbo,kuvujia kwa damu tumboni pamoja na maumivu ya tumbo.

-

Udongo/mchanga unaweza pia kuzuia ufyozwaji wa madini na virutubisho muhimu mwilini na inaweza pia kusababisha kupotea kwa hamu ya kula. Ikiwa mambo haya yatatokea,mtoto anaweza kukabiliwa na upungufu mkubwa wa virutubisho wezeshi kwa ukuaji wake

-

Ni vizuri kwa wanawake wajawazito wakijizuia kutumia udongo,pia ni muhimu kwao kufanya uchunguzi ikiwezekana pia kutilia maanani njia mbadala za kujipatia madini ya chuma badala ya kula udongo ili kujiepusha na matatizo yaliyoelezewa hapa. Hali hii (Pica) huweza kujitokeza kwa namna nyingi,wengine ikiwafanya wapende sana kula karatasi,barafu,sabuni,majivu,mkaa,magadi soda pamoja na nguo/matambara cr.afyainfo 

.

 KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!