TATIZO LA CHUNUSI KWENYE NGOZI

CHUNUSI

• • • • • •

HUSABABISHWA NA NINI?

Tezi zinazotengeneza mafuta(sebaceous glands) zipo katika kila kinyweleo(hair follicle) na hutengeneza mafuta ambayo hulainisha ngozi. Baadhi ya mafuta hurundikana(clogged), bakteria kuzaliana na mcharuko-mwili kutokea. Hii hutokea katika kipindi cha balehe(kati ya umri wa miaka 12-24), kipindi homoni za kiume hutolewa kwa wingi kwa wote wavulana na wasichana. Watu wachache pia huwa na chunusi nusu ya maisha yao yote


Sababu nyingine ni kama; Vyakula visivyokuwa na virutubisho muhimu(junk foods), Vidonge vya uzazi wa mpango, Vipodozi, Aleji/Mzio, Msongo wa mawazo, Kurithi, Vinyweleo vingi usoni, Hedhi zisizoeleweka n.k...

.

MAMBO GANI UNAWEZA KUFANYA KUZIDHIBITI?

KIUJUMLA

1. Usafi ni muhimu: Hakikisha ngozi yako inaoshwa vizuri na kuwa safi. 

2. Usibinye chunusi: Kama huwezi kutolewa chunusi kwa kifaa maalumu na mtaalamu, osha mikono yako na epuka kushika uso. Usiguse eneo la chunusi hadi mikono iwe safi


3. Safisha/fua foronya ya mto unaolalia mara kwa mara kwa sabuni zisizo na manukato


4. Hakikisha unapata miale ya jua usoni mwako kila siku: Pata hews safi na fanya mazoezi na pumzika vya kutosha ili kuondoa vijisumu(toxins)


5. Epuka kucharura(irritating) ngozi: Epuka nguo kuisugua ngozi katika maeneo yaliyoathirika. Usiongee na simu kwa kuiweka mashavuni kwa muda mrefu


6. Epuka msongo wa mawazo: Kwani huweza kupelekea mabadiliko ya homoni 

7. Usipake mafuta/make-up usoni: Haswa cream za grisi au manukato. 

8. Epuka dawa za steroid za kunywa au za kupaka kwani kuzidishwa hali hii kama; Hydrocortisone cream


9. Wanaume wanyoe ndevu kwa kiwembe kipya na wakate kuelekea mlalo wa ndevu zinapootea. Machine za kushevia husababisha makovu .

.

MAMBO MENGINE YA KUFANYA 

1. Weka kitambaa baridi(barafu) au cha moto

2. Sugua uso kwa majimaji ya Limau usiku na uoshe asubuhi

3. Unaweza changanya siki ya(apple cider) na maji na paka maeneo athirika. Hii huweza ku-balance pH ya ngozi

4. Kama una makovu tayari, paka nanasi fresh kwenye makovu na tumia vidonge vya bromelain 750mg kila siku

5. KAMA CHUNUSI ZAKO NI NYINGI KUPITA KIASI: Oga mvuke(steam bath) mara 2-3 kwa wiki


NAMNA BORA YA KULA:.........

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA MAWASILIANO NI +255758286584




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!